Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Zaburi 51:13 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

13 Nitawafundisha wakosaji njia zako, Na wenye dhambi watarejea kwako.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

13 Hapo nitawafunza wakosefu njia yako, nao wenye dhambi watarudi kwako.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

13 Hapo nitawafunza wakosefu njia yako, nao wenye dhambi watarudi kwako.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

13 Hapo nitawafunza wakosefu njia yako, nao wenye dhambi watarudi kwako.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

13 Ndipo nitakapowafundisha wakosaji njia zako, na wenye dhambi watarejea kwako.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

13 Ndipo nitakapowafundisha wakosaji njia zako, na wenye dhambi watakugeukia wewe.

Tazama sura Nakili




Zaburi 51:13
24 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa hiyo BWANA akawaghadhibikia Israeli sana, akawahamisha mbali na uso wake; wala hapana aliyesalia ila kabila la Yuda peke yake.


Basi BWANA akakikataa kizazi chote cha Israeli, akawatesa, na kuwatia katika mikono ya watu wenye kuwateka nyara, hata alipokwisha kuwatupa, watoke machoni pake.


hata BWANA akawaondoa Waisraeli wasiwe mbele zake, kama vile alivyosema kwa kinywa cha watumishi wake wote, manabii. Basi Waisraeli walichukuliwa mateka kutoka nchi yao wenyewe, waende nchi ya Ashuru, hata leo.


Sheria ya BWANA ni kamilifu, Huiburudisha nafsi. Ushuhuda wa BWANA ni amini, Humtia hekima mtu asiye nayo.


Miisho yote ya dunia itakumbuka, Na watu watamrejea BWANA; Jamaa zote za mataifa watamsujudia.


Ee BWANA, unijulishe njia zako, Unifundishe mapito yako,


BWANA yu mwema, mwenye adili, Kwa hiyo atawafundisha wenye dhambi njia.


Ndipo nikakuungamia dhambi yangu, Wala sikuuficha upotovu wangu. Nilisema, Nitayakiri maasi yangu kwa BWANA, Nawe ukanisamehe upotovu wa dhambi yangu.


Na mataifa mengi watakwenda na kusema, Njoni, twende juu mlimani kwa BWANA, nyumbani kwa Mungu wa Yakobo, naye atatufundisha njia zake, nasi tutakwenda katika mapito yake maana katika Sayuni itatoka sheria, na neno la BWANA katika Yerusalemu.


Zifanye akili za watu hawa zipumbae, na uyatie uzito masikio yao, na uyafumbe macho yao; wasije wakaona kwa macho yao, na kusikia kwa masikio yao, na kufahamu kwa mioyo yao, na kurejea na kuponywa.


Hakika nimemsikia Efraimu, akijililia hivi, Umeniadhibu, nami nikaadhibika, kama ndama asiyeizoea nira; unigeuze, nami nitageuka; kwa maana wewe u BWANA, Mungu wangu.


akasema, Amin, nawaambia, Msipoongoka na kuwa kama watoto, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni.


lakini nimekuombea wewe ili imani yako isipungue; nawe utakapoongoka waimarishe ndugu zako.


akasema, Ewe mwenye kujaa hila na uovu wote, mwana wa Ibilisi, adui wa haki yote, huachi kuzipotoa njia za Bwana zilizonyooka?


Basi, wakisafirishwa na kanisa, wakapita kati ya nchi ya Foinike na Samaria, wakitangaza habari za kuongoka kwao Mataifa; wakawafurahisha ndugu sana.


Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake Bwana;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo