Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Zaburi 48:10 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

10 Kama lilivyo jina lako, Ee Mungu, Ndivyo na sifa yako hadi miisho ya dunia. Mkono wako wa kulia umejaa haki;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

10 Jina lako lasifika kila mahali, sifa zako zaenea popote duniani. Kwa mkono wako umetenda kwa haki;

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

10 Jina lako lasifika kila mahali, sifa zako zaenea popote duniani. Kwa mkono wako umetenda kwa haki;

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

10 Jina lako lasifika kila mahali, sifa zako zaenea popote duniani. Kwa mkono wako umetenda kwa haki;

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

10 Ee Mungu, kama jina lako lilivyo, sifa zako zinafika hadi miisho ya dunia, mkono wako wa kuume umejazwa na haki.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

10 Ee Mungu, kama jina lako lilivyo, sifa zako zinafika hadi miisho ya dunia, mkono wako wa kuume umejazwa na haki.

Tazama sura Nakili




Zaburi 48:10
16 Marejeleo ya Msalaba  

Yeye, BWANA, ndiye Mungu wetu; Duniani kote kuna hukumu zake.


Kwa kuwa BWANA ni mwenye haki, Apenda matendo ya haki, Wanyofu wa moyo watauona uso wake.


Toka maawio ya jua hata machweo yake Jina la BWANA husifiwa.


BWANA ni mwenye haki katika njia zake zote, Na mwenye huruma katika matendo yake yote.


Umeipenda haki; Umeichukia dhuluma. Kwa hiyo MUNGU, Mungu wako, amekutia mafuta, Mafuta ya furaha kuliko wenzako.


Mfalme mkuu upendaye hukumu kwa haki; Umeiimarisha haki; Umefanya hukumu na haki katika Israeli.


usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kulia wa haki yangu.


Kwa maana tokea maawio ya jua hata machweo yake jina langu ni kuu katika mataifa; na katika kila mahali unatolewa uvumba na dhabihu safi kwa jina langu; maana jina langu ni kuu katika mataifa, asema BWANA wa majeshi.


Lakini na alaaniwe mtu adanganyaye, ambaye katika kundi lake ana dume, akaweka nadhiri, ila amtolea Bwana kitu kilicho na kilema; kwa maana mimi ni Mfalme mkuu, asema BWANA wa majeshi, na jina langu latisha katika mataifa.


Kama hutaki kutunza kufanya maneno yote ya torati hii yaliyoandikwa katika kitabu hiki, upate kulicha jina hili la fahari na utisho, BWANA, MUNGU WAKO;


Maana Wakanaani na wenyeji wote wa nchi hii watasikia habari hii, nao watatuzingira, na kulifuta jina letu katika nchi. Nawe utafanya nini kwa ajili ya jina lako kuu?


Kisha nikaziona mbingu zimefunuka, na tazama, farasi mweupe, na yeye aliyempanda, aitwaye Mwaminifu na Wa kweli, naye kwa haki ahukumu na kufanya vita.


kwa kuwa hukumu zake ni za kweli na haki; maana amemhukumu yule kahaba mkuu aliyeiharibu nchi kwa uasherati wake, na kuipatiliza damu ya watumwa wake mkononi mwake.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo