Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Zaburi 45:3 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

3 Jifungie upanga wako pajani, wewe uliye hodari, Utukufu ni wako na fahari ni yako.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

3 Jifunge upanga wako, ewe shujaa! Wewe ni mtukufu na mwenye fahari.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

3 Jifunge upanga wako, ewe shujaa! Wewe ni mtukufu na mwenye fahari.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

3 Jifunge upanga wako, ewe shujaa! Wewe ni mtukufu na mwenye fahari.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

3 Jifunge upanga wako pajani mwako, ee mwenye nguvu, jivike fahari na utukufu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

3 Jifunge upanga wako pajani mwako, ee mwenye nguvu, jivike fahari na utukufu.

Tazama sura Nakili




Zaburi 45:3
22 Marejeleo ya Msalaba  

Huyo alipokuwa angali akinena, akatokea na mwingine, na kusema, Moto wa Mungu umeanguka kutoka mbinguni na kuwateketeza kondoo, na wale watumishi, na kuwaangamiza; mimi peke yangu nimepona, mimi tu, kukuletea habari.


Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA. Wewe, BWANA, Mungu wangu, Umejifanya mkuu sana; Umejivika heshima na utukufu.


Ili kuwajulisha watu matendo yake makuu, Na utukufu wa fahari ya ufalme wake.


Nitaifikiri fahari ya utukufu wa adhama yako, Na matendo yako yote ya ajabu.


Utukufu wake ni mkuu kwa wokovu wako, Heshima na adhama waweka juu yake.


Kwa kuwa mfalme humtumainia BWANA, Na kwa fadhili zake Aliye Juu hatatikisika.


Heshima na adhama ziko mbele zake, Nguvu na uzuri zimo katika patakatifu pake.


Kama mpera kati ya miti ya msituni, Kadhalika mpendwa wangu kati ya vijana. Niliketi kivulini mwake kwa furaha, Na matunda yake niliyaonja kuwa matamu.


Mashavu yake ni kama matuta ya rihani Ambayo hufanyizwa manukato; Midomo yake ni kama nyinyoro, Inadondosha matone ya manemane;


Naye anifanya kinywa changu kuwa kama upanga mkali; katika kivuli cha mkono wake amenisitiri; naye amenifanya kuwa mshale uliosuguliwa; katika podo lake amenificha;


Neno lile alilowapelekea wana wa Israeli akihubiri Habari Njema ya amani kwa Yesu Kristo (ndiye Bwana wa wote),


Maana Kristo alikufa akawa hai tena kwa sababu hii, awamiliki waliokufa na walio hai pia.


Yeye kwa kuwa ni mng'ao wa utukufu wa Mungu na chapa kamili ya nafsi yake, akivichukua vyote kwa amri ya uweza wake, akiisha kufanya utakaso wa dhambi, aliketi katika mkono wa kulia wa Ukuu huko juu;


Maana neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena ni jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.


Basi, katika hayo tunayosema, neno lililo kuu ndilo hili: Tunaye kuhani mkuu wa namna hii, aliyeketi mkono wa kulia wa kiti cha enzi cha Ukuu mbinguni,


Yeye aliye Mungu pekee, Mwokozi wetu kwa Yesu Kristo Bwana wetu; utukufu una yeye, na ukuu, na uwezo, na nguvu, tangu milele, na sasa, na hata milele. Amina.


Naye alikuwa na nyota saba katika mkono wake wa kulia; na upanga mkali, wenye makali kuwili, ukitoka katika kinywa chake; na uso wake kama jua liking'aa kwa nguvu zake.


Na upanga mkali hutoka kinywani mwake ili kwa upanga huo awapige mataifa. Naye atawachunga kwa fimbo ya chuma, naye anakanyaga shinikizo la mvinyo ya ghadhabu ya hasira ya Mungu Mwenyezi.


na wale waliosalia waliuawa kwa upanga wake yeye aliyeketi juu ya yule farasi, upanga utokao katika kinywa chake. Na ndege wote wakashiba kwa nyama zao.


Ehudi alijifanyia upanga uliokuwa na makali kuwili, urefu wake ulipata dhiraa moja; akaufunga huo upanga ndani ya nguo yake katika paja lake la mkono wa kulia.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo