Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Zaburi 43:1 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

1 Ee Bwana, unihukumu, unitetee kwa taifa lisilo haki, Uniokoe kutoka kwa mtu wa hila asiye haki.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 Onesha kuwa sina hatia ee Mungu; utetee kisa changu dhidi ya watu wabaya; uniokoe na watu waongo na waovu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 Onesha kuwa sina hatia ee Mungu; utetee kisa changu dhidi ya watu wabaya; uniokoe na watu waongo na waovu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Onesha kuwa sina hatia ee Mungu; utetee kisa changu dhidi ya watu wabaya; uniokoe na watu waongo na waovu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Ee Mungu unihukumu, nitetee dhidi ya taifa lisilomcha Mungu, niokoe na watu wadanganyifu na waovu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Ee Mungu unihukumu, nitetee dhidi ya taifa lisilomcha Mungu, niokoe na watu wadanganyifu na waovu.

Tazama sura Nakili




Zaburi 43:1
21 Marejeleo ya Msalaba  

Mtu mmoja akamwambia Daudi ya kwamba, Ahithofeli yu katika hao waliopatana na Absalomu; Daudi akasema, Ee BWANA, nakusihi, uugeuze ushauri wa Ahithofeli uwe ubatili.


Kisha Absalomu akamwambia Ahithofeli, Haya, toa ushauri wako, tufanyeje.


Kwa maana vita vilienea huko juu ya uso wote wa nchi; na siku ile huo msitu ukala watu wengi kuliko wale walioliwa na upanga.


Wenye kiburi wamenifichia mtego na kamba; Wametandika wavu kando ya njia; Wameniwekea matanzi.


Ee BWANA, unihukumu mimi, Maana nimekwenda kwa ukamilifu wangu, Nami nimemtumaini BWANA bila wasiwasi.


Ee BWANA, uwapinge hao wanaonipinga, Upigane nao wanaopigana nami.


Unihukumu kwa haki yako, Ee BWANA, Mungu wangu, Na usiwaache wanisimange.


Utawaharibu wasemao uongo; BWANA humchukia mwuaji na mwenye hila


Kwa maana wageni wamenishambulia; Watu watishao wananitafuta nafsi yangu; Hawakumweka Mungu mbele yao.


Kusanyiko la mataifa na likuzunguke, Na juu yake uketi utawale.


BWANA atawaamua mataifa, BWANA, unihukumu mimi, Kwa kadiri ya haki yangu, Kulingana na unyofu nilio nao.


Ubaya wao wasio haki na ukome, Lakini umthibitishe mwenye haki. Kwa maana mjaribu mioyo na fikira Ndiye Mungu aliye mwenye haki.


Ee Mungu wangu, uniponye mkononi mwa mkorofi, Katika mkono wake mwovu na mdhalimu,


Bali Mungu ndiye ahukumuye; Humdhili huyu na kumwinua huyu.


Kwa sababu BWANA atawatetea; Naye atawateka uhai wao waliowateka.


Kwa sababu mkombozi wao ana nguvu; Atawatetea juu yako.


Nitaivumilia ghadhabu ya BWANA, kwa kuwa nimemwasi; hata atakaponitetea shutuma yangu, na kunifanyia hukumu; atanileta nje kwenye nuru, nami nitaiona haki yake.


Maana sijui sababu ya kujishitaki nafsi yangu, lakini sihesabiwi haki kwa ajili hiyo; ila anihukumuye mimi ni Bwana.


Yeye alipotukanwa, hakurudisha matukano; alipoteswa, hakutisha; bali alijikabidhi kwake yeye ahukumuye kwa haki.


Basi BWANA atuamue, akatuhukumu mimi na wewe, akaone, akanitetee neno langu, akaniokoe kutokana na mkono wako.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo