Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Zaburi 42:9 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

9 Nitamwambia Mungu, mwamba wangu, Kwa nini umenisahau? Kwa nini ninakwenda nikihuzunika, adui wakinionea?

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

9 Namwambia Mungu, mwamba wangu: “Kwa nini umenisahau? Yanini niende huko na huko nikiomboleza kwa kudhulumiwa na adui yangu?”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

9 Namwambia Mungu, mwamba wangu: “Kwa nini umenisahau? Yanini niende huko na huko nikiomboleza kwa kudhulumiwa na adui yangu?”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

9 Namwambia Mungu, mwamba wangu: “Kwa nini umenisahau? Yanini niende huko na huko nikiomboleza kwa kudhulumiwa na adui yangu?”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

9 Ninamwambia Mungu Mwamba wangu, “Kwa nini umenisahau? Kwa nini niendelee kuomboleza, nikiteswa na adui?”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

9 Ninamwambia Mungu Mwamba wangu, “Kwa nini umenisahau? Kwa nini niendelee kuomboleza, nikiwa nimeonewa na adui?”

Tazama sura Nakili




Zaburi 42:9
19 Marejeleo ya Msalaba  

Ee BWANA, utanisahau hadi lini, hata milele? Hadi lini utanificha uso wako?


BWANA ni jabali langu, na boma langu, na mwokozi wangu, Mungu wangu, mwamba wangu ninayemkimbilia, Ngao yangu, na pembe ya wokovu wangu, na ngome yangu.


Ee BWANA, nitakuita Ewe, mwamba wangu, Usiwe kwangu kama kiziwi. Nisije nikafanana nao washukao shimoni, Ikiwa umeninyamalia.


Nimejipinda na kuinama sana, Mchana kutwa ninaenda nikiomboleza.


Kwa kuwa Wewe ndiwe Mungu uliye nguvu zangu; kwa nini umenitupa? Kwa nini ninakwenda nikihuzunika, adui wakinionea?


Kwa sababu ya sauti ya adui, Kwa sababu ya dhuluma yake yule mwovu. Kwa maana wananitupia uovu, Na kwa ghadhabu wananiudhi.


Yeye tu ndiye mwamba wangu na wokovu wangu, Ngome yangu, sitatikisika.


Mungu amesahau fadhili zake? Amezuia kwa hasira rehema zake?


Wakakumbuka kuwa Mungu ni mwamba wao, Na Mungu Aliye Juu ni mkombozi wao.


Jicho langu limefifia kwa ajili ya mateso BWANA, ninakuita kila siku; Ninakunyoshea Wewe mikono yangu.


Kwa chombo chenye nyuzi kumi, Na kwa kinanda, Na kwa mlio wa kinubi.


Kisha nikarudi na kuona udhalimu wote unaotendeka chini ya jua; na tazama, machozi yao waliodhulumiwa, ambao walikuwa hawana mfariji; na upande wa wale waliowadhulumu kulikuwa na uwezo, lakini wale walikuwa hawana mfariji.


Mbona unasema, Ee Yakobo, mbona unanena, Ee Israeli, Njia yangu imefichwa, BWANA asiione, na hukumu yangu imempita Mungu wangu asiiangalie?


Je! Mwanamke aweza kumsahau mtoto wake anyonyaye, hata asimhurumie mwana wa tumbo lake? Naam, hawa waweza kusahau, lakini mimi sitakusahau wewe.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo