Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Zaburi 42:8 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

8 Mchana BWANA ataagiza fadhili zake, na usiku wimbo wake utakuwa nami, Naam, maombi kwa Mungu aliye uhai wangu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

8 Mwenyezi-Mungu atanijalia fadhili zake mchana; nami nimwimbie wimbo wa sifa usiku, nimwombe Mungu anipaye uhai.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

8 Mwenyezi-Mungu atanijalia fadhili zake mchana; nami nimwimbie wimbo wa sifa usiku, nimwombe Mungu anipaye uhai.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

8 Mwenyezi-Mungu atanijalia fadhili zake mchana; nami nimwimbie wimbo wa sifa usiku, nimwombe Mungu anipaye uhai.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

8 Mwenyezi Mungu huelekeza upendo wake mchana, wimbo wake uko nami usiku: maombi kwa Mungu wa uzima wangu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

8 Mchana bwana huelekeza upendo wake, usiku wimbo wake uko nami: maombi kwa Mungu wa uzima wangu.

Tazama sura Nakili




Zaburi 42:8
20 Marejeleo ya Msalaba  

Maana mawimbi ya mauti yalinizunguka, Mafuriko ya uovu yakanitia hofu.


Wala hapana asemaye, Yuko wapi Mungu Muumba wangu, Awapaye nyimbo wakati wa usiku;


Papo hapo maji yangalitugharikisha, Mto ungalipita juu ya roho zetu;


Ni kama umande wa Hermoni ushukao milimani pa Sayuni. Maana huko ndiko BWANA alikoamuru baraka, Naam, uzima hata milele.


Watauwa na waushangilie utukufu, Waimbe kwa sauti kuu vitandani mwao.


Nitamhimidi BWANA aniongozaye, Wakati wa usiku pia moyo wangu hunishauri.


BWANA ni nuru yangu na wokovu wangu, Nimwogope nani? BWANA ni ngome ya uzima wangu, Nimhofu nani?


Kimbilio langu utanilinda nisipate mateso, Utanizungusha nyimbo za kufurahia wokovu wangu.


Ee Mungu, Wewe ndiwe mfalme wangu, Uagize mambo ya wokovu kwa Yakobo.


Atanitumia msaada toka mbinguni na kuniokoa, Atawaaibisha wale wanaotaka kunishambulia. Mungu atazituma Fadhili zake na kweli yake.


Ninapokukumbuka kitandani mwangu, Ninakutafakari usiku kucha.


Nanena na moyo wangu usiku, Nawaza moyoni mwangu, Roho yangu naipeleleza.


Wanijuao umewatenga nami; Umenifanya kuwa chukizo kwao; Nimefungwa wala siwezi kutoka.


Mtakuwa na wimbo kama vile wakati wa usiku, ishikwapo sikukuu takatifu, mtakuwa na furaha ya moyo kama vile mtu aendapo na filimbi katika mlima wa BWANA, aliye Mwamba wa Israeli.


ndipo nitawaamria baraka yangu iwe juu yenu mwaka wa sita, nayo inchi itazaa matunda ya kutosha miaka mitatu.


Nami nikasema, Nimetupwa mbali na macho yako; Lakini nitatazama tena kukabili hekalu lako takatifu.


Yule afisa akamjibu, akasema, Bwana, mimi sistahili wewe uingie chini ya dari yangu; lakini sema neno tu, na mtumishi wangu atapona.


Lakini ilipokuwa karibu usiku wa manane Paulo na Sila walikuwa wakimwomba Mungu na kumwimbia nyimbo za kumsifu, na wafungwa wengine walikuwa wakiwasikiliza.


BWANA ataiamuru baraka ije juu yako katika ghala zako, na mambo yote utakayotia mkono wako; naye atakubarikia katika nchi akupayo BWANA, Mungu wako.


Kwa maana mlikufa, na uhai wenu umefichwa pamoja na Kristo katika Mungu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo