Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Zaburi 40:2 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

2 Akanipandisha toka shimo la uharibifu, Toka udongo wa utelezi; Akaisimamisha miguu yangu mwambani, Akaziimarisha hatua zangu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

2 Aliniondoa katika shimo la hatari, alinitoa katika matope ya dimbwi, akanisimamisha salama juu ya mwamba, na kuziimarisha hatua zangu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

2 Aliniondoa katika shimo la hatari, alinitoa katika matope ya dimbwi, akanisimamisha salama juu ya mwamba, na kuziimarisha hatua zangu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

2 Aliniondoa katika shimo la hatari, alinitoa katika matope ya dimbwi, akanisimamisha salama juu ya mwamba, na kuziimarisha hatua zangu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

2 Akanipandisha kutoka shimo la uharibifu, kutoka matope na utelezi; akaiweka miguu yangu juu ya mwamba na kunipa mahali imara pa kusimama.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

2 Akanipandisha kutoka shimo la uharibifu, kutoka matope na utelezi; akaiweka miguu yangu juu ya mwamba na kunipa mahali imara pa kusimama.

Tazama sura Nakili




Zaburi 40:2
24 Marejeleo ya Msalaba  

Kamba za mauti zilinizunguka, Shida za kuzimu zilinipata. Nilipata dhiki na mateso;


Uzielekeze hatua zangu kwa neno lako, Uovu usije ukanimiliki.


Maana adui ameifuatia nafsi yangu, Ameutupa chini uzima wangu. Amenikalisha mahali penye giza, Kama watu waliokufa zamani.


Nyayo zangu zimeshikamana na njia zako, Hatua zangu hazikuondoshwa.


Umezipanulia nafasi hatua zangu, Na miguu yangu haikuteleza.


Ndipo nchi iliyotikisika na kutetemeka, Misingi ya milima ikatingizika; Ikatikisika kwa sababu alikuwa na ghadhabu.


Maana atanisitiri bandani mwake siku ya mabaya, Atanisitiri katika sitara ya hema yake, Na kuniinua juu ya mwamba.


Hatua za mtu mwema huimarishwa na BWANA, Naye huipenda njia yake.


Toka mwisho wa nchi nitakulilia ninapozimia moyo, Uniongoze juu ya mwamba nisioweza kuupanda.


Ninazama katika matope mengi, Pasipowezekana kusimama. Nimefika penye maji ya vilindi, Mkondo wa maji unanigharikisha.


Wewe, uliyetuonesha mateso mengi, mabaya, Utatuhuisha tena. Utatupandisha juu tena Kutoka katika vina virefu chini ya nchi.


Maana fadhili zako kwangu ni nyingi sana; Umeiopoa nafsi yangu na kuzimu.


nao watakusanywa pamoja kama vile wakusanywavyo wafungwa katika shimo nao watafungwa katika gereza; na baada ya muda wa siku nyingi wataadhibiwa.


Na kwa habari zako wewe, kwa sababu ya damu ya agano lako, nimewatoa wafungwa wako katika shimo lile lisilo na maji.


na kuwatupa katika tanuri ya moto; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.


ambaye Mungu alimfufua, akiufungua uchungu wa mauti, kwa sababu haikuwezekana ashikwe nao.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo