Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Zaburi 39:6 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

6 Kweli, watu wote hupita kama kivuli; Wao hujisumbua bure tu; Wanajirundikia mali wala hawajui ni nani atakayeirithi.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

6 Kweli, kila mtu anapita kama kivuli; jitihada zake zote ni bure tu; anakusanya mali, asijue atakayeipata!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

6 Kweli, kila mtu anapita kama kivuli; jitihada zake zote ni bure tu; anakusanya mali, asijue atakayeipata!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

6 Kweli, kila mtu anapita kama kivuli; jitihada zake zote ni bure tu; anakusanya mali, asijue atakayeipata!

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

6 Hakika kila binadamu ni kama njozi aendapo huku na huko: hujishughulisha na mengi, lakini ni ubatili; anakusanya mali nyingi, wala hajui ni nani atakayejifaidi nayo.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

6 Hakika kila binadamu ni kama njozi aendapo huku na huko: hujishughulisha na mengi lakini ni ubatili; anakusanya mali nyingi, wala hajui ni nani atakayeifaidi.

Tazama sura Nakili




Zaburi 39:6
31 Marejeleo ya Msalaba  

Mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke Siku zake za kuishi si nyingi, naye hujaa taabu.


Ninadhoofika; sitaishi sikuzote; Usinisumbue, kwani siku zangu ni uvuvio.


Kumbuka ya kwamba maisha yangu ni upepo; Jicho langu halitaona mema tena.


Kazi yenu ni bure, mnaoamka mapema, Na kukawia kwenda kulala, Na kula chakula cha taabu; Yeye humpa mpenzi wake usingizi.


Binadamu ni kama ubatili, Siku zake ni kama kivuli kipitacho.


Ni mwanamume gani atakayeishi asione mauti, Atakayejiokoa nafsi yake na mkono wa kuzimu?


Mtu mwema huwaachia wana wa wanawe urithi; Na mali ya mkosaji huwa akiba kwa mwenye haki.


Je! Utavikazia macho vile ambavyo si kitu? Maana bila shaka mali hujifanyia mabawa, Kama tai arukaye mbinguni.


Kwa maana mali haziwi za milele; Na taji je! Ladumu tangu kizazi hata kizazi?


Nimeziona kazi zote zifanywazo chini ya jua; na, tazama, mambo yote ni ubatili na kufukuza upepo.


Kwa hiyo ondoa majonzi moyoni mwako, nawe uuondoe ubaya mwilini mwako; kwa maana ujana ni ubatili, na utu uzima pia.


Hii ndiyo jumla ya maneno; yote yamekwisha sikiwa; Mche Mungu, nawe uzishike amri zake, Maana kwa jumla ndiyo impasayo mtu.


Mhubiri asema, Ubatili mtupu; mambo yote ni ubatili!


Kwa sababu Mungu humpa yeye aliyemridhia hekima na maarifa na furaha; bali mkosaji humpa taabu, ili kukusanya na kututa, apate kumpa huyo ambaye Mungu amridhia. Hayo nayo ni ubatili na kufukuza upepo.


tena nikajikusanyia fedha na dhahabu, na tunu za kifalme na za kutoka katika majimbo. Nikajipatia waimbaji, wanaume kwa wanawake, nao wale ambao wanadamu wanawatunuka, masuria wengi sana.


na mali hizo zimepotea kwa bahati mbaya; naye akiwa amezaa mwana, hamna kitu mkononi mwake.


Kwa nini mtoe fedha kwa ajili ya kitu ambacho si chakula? Na mapato yenu kwa kitu kisichoshibisha? Nisikilizeni kwa bidii, mle kilicho chema, Na kujifurahisha nafsi zenu kwa unono.


Basi, ikiwa hamwezi hata neno lililo dogo, kwa nini kujisumbua kwa ajili ya yale mengine?


Ninyi msitafute mtakavyokula wala mtakavyokunywa; wala msiwe na wasiwasi,


Na wale wautumiao ulimwengu huu, kama hawautumii sana; kwa maana mambo ya ulimwengu huu yanapita.


lakini hamjui yatakayokuwako kesho. Uzima wenu ni nini? Maana ninyi ni mvuke uonekanao kwa muda mfupi tu, kisha hutoweka.


Dhahabu yenu na fedha yenu zimeingia kutu, na kutu yake itawashuhudia, nayo itakula miili yenu kama moto. Mmejiwekea akiba katika siku za mwisho.


Maana, Mwili wote ni kama majani, Na fahari yake yote ni kama ua la majani. Majani hukauka na ua lake huanguka;


huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo