Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Zaburi 39:12 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

12 Ee BWANA, usikie maombi yangu, Utege sikio lako niliapo, Usiyapuuze machozi yangu. Kwa maana mimi ni mgeni wako, Msafiri kama baba zangu wote.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

12 Usikie sala yangu, ee Mwenyezi-Mungu; usikilize kilio changu, usikae kimya ninapolia. Maana, mimi ni kama mgeni tu apitaye, ni msafiri kama walivyokuwa wazee wangu wote.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

12 Usikie sala yangu, ee Mwenyezi-Mungu; usikilize kilio changu, usikae kimya ninapolia. Maana, mimi ni kama mgeni tu apitaye, ni msafiri kama walivyokuwa wazee wangu wote.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

12 Usikie sala yangu, ee Mwenyezi-Mungu; usikilize kilio changu, usikae kimya ninapolia. Maana, mimi ni kama mgeni tu apitaye, ni msafiri kama walivyokuwa wazee wangu wote.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

12 “Ee Mwenyezi Mungu, usikie maombi yangu, usikie kilio changu unisaidie, usiwe kiziwi kwa kulia kwangu. Kwani mimi ninaishi na wewe kama mgeni, mhamiaji, kama walivyokuwa baba zangu wote,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

12 “Ee bwana, usikie maombi yangu, usikie kilio changu unisaidie, usiwe kiziwi kwa kulia kwangu. Kwani mimi ninaishi na wewe kama mgeni, kama walivyokuwa baba zangu wote,

Tazama sura Nakili




Zaburi 39:12
19 Marejeleo ya Msalaba  

Abrahamu akaishi kama mgeni kwa Wafilisti siku nyingi.


Yakobo akamjibu Farao, Siku za kuishi kwangu ni miaka mia moja na thelathini; siku za maisha yangu zimekuwa chache, tena za taabu, wala hazikufikia siku za maisha ya baba zangu katika siku za kuishi kwao.


Labda BWANA atayaangalia mabaya yaliyonipata, naye BWANA atanilipa mema kwa sababu ya kunilaani kwake leo.


Rudi, ukamwambie Hezekia, mkuu wa watu wangu, BWANA, Mungu wa Daudi baba yako asema hivi, Nimeyasikia maombi yako, na kuyaona machozi yako; tazama, nitakuponya; siku ya tatu utapanda nyumbani kwa BWANA.


Kwani sisi tu wageni na wapitaji mbele zako, kama walivyokuwa baba zetu wote; siku zetu duniani ni kama kivuli, na hakuna tumaini la kuishi.


Nijapokuwa ni kama kitu kilichooza, kinachosinyaa, Mfano wa nguo iliyoliwa na nondo.


Rafiki zangu hunidharau; Lakini jicho langu humwagia Mungu machozi;


Ee BWANA, usikie kuomba kwangu, Kilio changu kikufikie.


Kamba za mauti zilinizunguka, Shida za kuzimu zilinipata. Nilipata dhiki na mateso;


Mimi ni mgeni katika nchi, Usinifiche maagizo yako.


Amri zako zimekuwa nyimbo zangu, Katika nyumba yangu ya ugenini.


Umehesabu kutangatanga kwangu; Uyatie machozi yangu katika chupa yako; (Je! Hayamo katika kitabu chako?)


Maana kwa hasira yako maisha yetu yanapita punde, Maisha yetu yanaisha kama kite.


Nayo nchi haitauzwa kabisa kabisa; kwani nchi ni yangu mimi; maana ninyi ni wageni na wapangaji wangu.


Basi siku zote tuna moyo mkuu; tena twajua ya kuwa, wakati tuwapo hapa katika mwili, tunakaa mbali na Bwana.


Hawa wote wakafa katika imani, walikuwa hawajazipokea zile ahadi, bali wakaziona tokea mbali na kuzishangilia, na kukiri kwamba walikuwa wageni, na wasafiri juu ya nchi.


Yeye, siku hizo za mwili wake, alimtolea yule, awezaye kumwokoa na kumtoa katika mauti, maombi na dua pamoja na kulia sana na machozi, akasikilizwa kwa jinsi alivyokuwa mcha Mungu;


Na ikiwa mnamwita Baba, yeye ahukumuye kila mtu pasipo upendeleo, kwa kadiri ya kazi yake, nendeni kwa hofu katika wakati wenu wa kukaa hapa kama wageni.


Wapenzi, nawasihi kama wapitaji na wasafiri, ziepukeni tamaa za mwili zipiganazo na roho.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo