Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Zaburi 37:3 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

3 Umtumaini BWANA ukatende mema, Ukae katika nchi, upendezwe na uaminifu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

3 Mtumainie Mwenyezi-Mungu na kutenda mema, upate kuishi katika nchi na kuwa salama.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

3 Mtumainie Mwenyezi-Mungu na kutenda mema, upate kuishi katika nchi na kuwa salama.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

3 Mtumainie Mwenyezi-Mungu na kutenda mema, upate kuishi katika nchi na kuwa salama.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

3 Mtumaini Mwenyezi Mungu na utende yaliyo mema. Kaa katika nchi ukafurahie malisho salama.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

3 Mtumaini bwana na utende yaliyo mema; Kaa katika nchi ukafurahie malisho salama.

Tazama sura Nakili




Zaburi 37:3
20 Marejeleo ya Msalaba  

BWANA akamtokea, akasema, Usishuke kwenda Misri, kaa katika nchi nitakayokuambia.


Kaa ugenini katika nchi hiyo, nami nitakuwa pamoja nawe, na kukubariki, maana nitakupa wewe na uzao wako nchi hizi zote. Nami nitakifanya imara kiapo nilichomwapia Abrahamu baba yako.


Akatazama, kumbe! Pana mkate umeokwa juu ya makaa, na gudulia la maji, kichwani pake. Akala, akanywa, akajinyosha tena.


Ee BWANA, unihukumu mimi, Maana nimekwenda kwa ukamilifu wangu, Nami nimemtumaini BWANA bila wasiwasi.


Ili kuwaponya nafsi zao kutoka kwa mauti, Na kuwahuisha wakati wa njaa.


Toeni dhabihu za haki, Na kumtumaini BWANA.


Enyi watu, mtumainini sikuzote, Ifunueni mioyo yenu mbele zake; Mungu ndiye kimbilio letu.


Mtumaini BWANA kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe;


Atalilisha kundi lake kama mchungaji, Atawakusanya wana-kondoo mikononi mwake; Na kuwachukua kifuani mwake, Nao wanyonyeshao atawaongoza polepole.


Ni nani miongoni mwenu amchaye BWANA, aitiiye sauti ya mtumishi wake? Yeye aendaye katika giza, wala hana nuru, naye alitumainia jina la BWANA, na kumtegemea Mungu wake.


Akawauliza, Je! Hapo nilipowatuma hamna mfuko, wala mkoba, wala viatu, mlipungukiwa na kitu? Wakasema, La!


kumpenda BWANA, Mungu wako, kuitii sauti yake, na kushikamana naye; kwani hiyo ndiyo uzima wako, na wingi wa siku zako; upate kukaa katika nchi BWANA aliyowaapia baba zako, Abrahamu, na Isaka, na Yakobo, kuwa atawapa.


Basi sasa, nakusihi, bwana wangu, mfalme, na asikie maneno ya mtumishi wake. Ikiwa ni BWANA aliyekuchochea juu yangu, na akubali sadaka; bali ikiwa ni wanadamu, na walaaniwe mbele za BWANA; kwa sababu wamenifukuza leo, nisishikamane na urithi wa BWANA, wakisema, Nenda, ukatumikie miungu mingine.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo