Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Zaburi 35:27 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

27 Washangilie na kufurahi, Wapendezwao na haki yangu. Naam, waseme daima, Atukuzwe BWANA, Apendezwaye na amani ya mtumishi wake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

27 Lakini wanaotaka kuona kuwa sina hatia, wapaaze sauti kwa furaha waseme daima: “Mwenyezi-Mungu ni mkuu mno! Hupendezwa na fanaka ya mtumishi wake.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

27 Lakini wanaotaka kuona kuwa sina hatia, wapaaze sauti kwa furaha waseme daima: “Mwenyezi-Mungu ni mkuu mno! Hupendezwa na fanaka ya mtumishi wake.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

27 Lakini wanaotaka kuona kuwa sina hatia, wapaaze sauti kwa furaha waseme daima: “Mwenyezi-Mungu ni mkuu mno! Hupendezwa na fanaka ya mtumishi wake.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

27 Wale wanaofurahia hukumu yangu ya haki wapige kelele za shangwe na furaha; hebu waseme siku zote, “Mwenyezi Mungu atukuzwe, ambaye amefurahia mafanikio ya mtumishi wake.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

27 Wale wanaofurahia hukumu yangu ya haki wapige kelele za shangwe na furaha; hebu waseme siku zote, “bwana atukuzwe, ambaye amefurahia mafanikio ya mtumishi wake.”

Tazama sura Nakili




Zaburi 35:27
20 Marejeleo ya Msalaba  

Na makuhani wake nitawavika wokovu, Na watauwa wake watashangilia.


Makuhani wako na wavikwe haki, Watauwa wako na washangilie.


Uitoe nafsi yangu kifungoni. Nipate kulishukuru jina lako. Wenye haki watanizunguka, Kwa kuwa Wewe unanikirimu.


BWANA huwaridhia wao wamchao, Na kuzitarajia fadhili zake.


Kwa kuwa BWANA awaridhia watu wake, Huwapamba wenye upole kwa wokovu.


Mfurahieni BWANA; Shangilieni, enyi wenye haki Pigeni vigelegele vya furaha; Ninyi nyote mlio wanyofu wa moyo.


Nilimtafuta BWANA, naye akanijibu, Akaniokoa kutoka kwa hofu zangu zote.


Washangilie na wakufurahie, Wote wakutafutao. Waupendao wokovu wako Waseme daima, BWANA ni Mkuu.


Nami ni maskini na mhitaji, Bwana atanitunza. Ndiwe msaada wangu na mwokozi wangu, Ee Mungu wangu, usikawie.


Bali wenye haki hufurahi, Na kuushangilia uso wa Mungu, Naam, hupiga kelele kwa furaha.


Washangilie, wakufurahie, Wote wakutafutao. Waupendao wokovu wako Waseme daima, Atukuzwe Mungu.


Kwa maana umenifanyia hukumu na haki Umeketi kitini pa enzi ukihukumu kwa haki.


Utajiri na heshima ziko kwangu, Naam, utajiri udumuo, na haki pia.


Imba, Ee binti Sayuni; piga kelele, Ee Israeli; Furahi na kushangilia kwa moyo wako wote, Ee binti Yerusalemu.


BWANA, Mungu wako, yuko katikati yako shujaa awezaye kuokoa; Atakushangilia kwa furaha kuu, Atakutuliza katika upendo wake, Atakufurahia kwa kuimba.


Basi ninyi hivi sasa mna huzuni; lakini mimi nitawaona tena; na mioyo yenu itafurahi, na furaha yenu hakuna awaondoleaye.


Furahini pamoja nao wafurahio; lieni pamoja nao waliao.


Na kiungo kimoja kikiumia, viungo vyote huumia nacho, na kiungo kimoja kikitukuzwa, viungo vyote hufurahi pamoja nacho.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo