Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Zaburi 35:13 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

13 Bali mimi, walipougua wao, Nguo yangu ilikuwa gunia. Nilijitesa nafsi yangu kwa kufunga; Maombi yangu yakarejea kifuani mwangu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

13 Lakini wao walipokuwa wagonjwa, mimi nilivaa magunia kuonesha huzuni; nilijitesa kwa kujinyima chakula. Nilisali nikiwa nimeinamisha kichwa,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

13 Lakini wao walipokuwa wagonjwa, mimi nilivaa magunia kuonesha huzuni; nilijitesa kwa kujinyima chakula. Nilisali nikiwa nimeinamisha kichwa,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

13 Lakini wao walipokuwa wagonjwa, mimi nilivaa magunia kuonesha huzuni; nilijitesa kwa kujinyima chakula. Nilisali nikiwa nimeinamisha kichwa,

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

13 Lakini walipokuwa wagonjwa, nilivaa gunia na nikajinyenyekeza kwa kufunga. Maombi yangu yaliponirudia bila kujibiwa,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

13 Lakini walipokuwa wagonjwa, nilivaa nguo ya gunia na nikajinyenyekesha kwa kufunga. Maombi yangu yaliponirudia bila kujibiwa,

Tazama sura Nakili




Zaburi 35:13
13 Marejeleo ya Msalaba  

Je! Mimi sikulia kwa ajili ya huyo aliyekuwa katika taabu? Nafsi yangu, je! Haikusononeka kwa ajili ya wahitaji?


Waketio langoni hunisema, Na nyimbo za walevi hunidhihaki.


Husema, Mbona tumefunga, lakini huoni? Mbona tumejitaabisha nafsi zetu, lakini huangalii? Fahamuni, siku ya kufunga kwenu mnatafuta anasa zenu wenyewe, na kuwalemea wote watendao kazi kwenu.


Je! Kufunga namna hii ni saumu niliyoichagua mimi? Je! Ni siku ya mtu kujitaabisha nafsi yake? Ni kuinama kichwa kama unyasi, na kutanda nguo za magunia na majivu chini yake? Je! Utasema ni siku ya kufunga, na ya kukubaliwa na BWANA?


Amri hii itakuwa amri ya milele kwenu; katika mwezi wa saba, siku ya kumi ya mwezi, mtajinyima, msifanye kazi ya namna yoyote, mzalia na mgeni akaaye kati yenu.


Ni Sabato ya raha ya makini kwenu nanyi mtajinyima; ni amri ya milele.


Na nyumba ile ikistahili, amani yenu na iifikie; la, kwamba haistahili, amani yenu na iwarudie ninyi.


lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi,


na akiwamo mwana wa amani, amani yenu itamkalia; lakini kama hamna, amani yenu itarudi kwenu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo