Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Zaburi 33:4 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

4 Kwa kuwa neno la BWANA lina adili, Na kazi yake yote huitenda kwa uaminifu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

4 Neno la Mwenyezi-Mungu ni la kweli; na matendo yake yote ni ya kuaminika.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

4 Neno la Mwenyezi-Mungu ni la kweli; na matendo yake yote ni ya kuaminika.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

4 Neno la Mwenyezi-Mungu ni la kweli; na matendo yake yote ni ya kuaminika.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

4 Maana neno la Mwenyezi Mungu ni haki na kweli, ni mwaminifu kwa yote atendayo.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

4 Maana neno la bwana ni haki na kweli, ni mwaminifu kwa yote atendayo.

Tazama sura Nakili




Zaburi 33:4
17 Marejeleo ya Msalaba  

Akasema, Na atukuzwe BWANA, Mungu wa bwana wangu Abrahamu, ambaye hakuacha rehema zake na kweli yake kwa bwana wangu. BWANA akaniongoza mimi nami njiani hata nyumba ya nduguze bwana wangu.


Maana nayafuata mausia yako yote, kuwa ya adili, Kila njia ya uongo naichukia.


Najua ya kuwa hukumu zako ni za haki, Ee BWANA, na kwa uaminifu umenitesa.


Maneno ya BWANA ni maneno safi, Ni fedha iliyojaribiwa kalibuni juu ya nchi; Iliyosafishwa mara saba.


Maagizo ya BWANA ni ya adili, Huufurahisha moyo. Amri ya BWANA ni safi, Huyatia macho nuru.


Njia zote za BWANA ni fadhili na kweli, Kwao walishikao agano lake na shuhuda zake.


Mbele za BWANA, kwa maana anakuja, Kwa maana anakuja aihukumu nchi. Atauhukumu ulimwengu kwa haki, Na mataifa kwa uaminifu wake.


Kila neno la Mungu limehakikishwa; Yeye ni ngao yao wamwaminio.


Basi mimi, Nebukadneza, namhimidi Mfalme wa mbinguni, namtukuza na kumheshimu; maana matendo yake yote ni kweli, na njia zake ni za adili; na wale waendao kwa kutakabari, yeye aweza kuwadhili.


Je! Litasemwa neno hili, enyi nyumba ya Yakobo, Roho ya BWANA imepunguzwa? Je! Haya ni matendo yake? Je! Maneno yangu hayamfai yeye aendaye kwa unyofu?


Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.


Basi torati ni takatifu, na ile amri ni takatifu, na ya haki, na njema.


Yeye Mwamba, kazi yake ni kamilifu; Maana, njia zake zote ni haki. Mungu wa uaminifu, asiye na uovu, Yeye ndiye mwenye haki na adili.


katika tumaini la uzima wa milele, ambao Mungu asiyeweza kusema uongo aliuahidi tangu milele;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo