Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Zaburi 32:3 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

3 Nilipokosa kuungama dhambi zangu, mifupa yangu ilipooza Kwa kulia kwangu mchana kutwa.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

3 Wakati nilipokuwa sijakiri dhambi yangu, nilikuwa nimedhoofika kwa kulia mchana kutwa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

3 Wakati nilipokuwa sijakiri dhambi yangu, nilikuwa nimedhoofika kwa kulia mchana kutwa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

3 Wakati nilipokuwa sijakiri dhambi yangu, nilikuwa nimedhoofika kwa kulia mchana kutwa.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

3 Niliponyamaza, mifupa yangu ilichakaa kwa kulia kwa maumivu makali mchana kutwa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

3 Niliponyamaza, mifupa yangu ilichakaa kwa kulia kwa maumivu makali mchana kutwa.

Tazama sura Nakili




Zaburi 32:3
26 Marejeleo ya Msalaba  

Hata maombolezo hayo yalipokwisha, Daudi akatuma mtu, akamtwaa, akamtia nyumbani mwake; naye akawa mkewe, akamzalia mtoto wa kiume. Lakini jambo lile alilolitenda Daudi likamchukiza BWANA.


Kwani kuugua kwangu kwaja kana kwamba ni chakula, Na kunguruma kwangu kumemiminika kama maji.


Wakati wa usiku mifupa yangu huchomeka ndani yangu, Na maumivu yanayonitafuna hayapumziki.


Ngozi yangu ni nyeusi, nayo yanitoka, Na mifupa yangu imeteketea kwa joto.


Mungu wangu, Mungu wangu, Mbona umeniacha? Mbona U mbali na wokovu wangu, Na maneno ya kuugua kwangu?


Hamna uzima katika mwili wangu Kwa sababu ya ghadhabu yako. Wala hamna amani mifupani mwangu Kwa sababu ya hatia zangu.


Nimedhoofika na kupondeka sana, Nimeugua kwa fadhaa ya moyo wangu.


Unifanye kusikia furaha na shangwe, Mifupa uliyoiponda ifurahi.


BWANA, unifadhili, maana ninanyauka; BWANA, uniponye, mifupa yangu imefadhaika.


Moyo uliochangamka ni dawa nzuri; Bali roho iliyopondeka huikausha mifupa.


Afichaye dhambi zake hatafanikiwa; Bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema.


Wana wako wamezimia, Wamelala penye pembe za njia kuu zote Kama kulungu wavuni; Wamejaa hasira ya BWANA, Lawama ya Mungu wako.


Kwa sababu ya uovu wa kutamani kwake niliona hasira, nikampiga; nilificha uso wangu, nikaona ghadhabu; naye akaendelea kwa ukaidi, kuifuata njia ya moyo wake mwenyewe.


Sisi sote twanguruma kama dubu; twaomboleza kama hua; twatazamia hukumu ya haki, lakini hapana; na wokovu, lakini u mbali nasi.


Yuda amehamishwa kwa sababu ya kuonewa, Na kwa sababu ya utumwa mkuu; Anakaa kati ya mataifa, Haoni raha yoyote; Wote waliomfuata wamempata Katika dhiki yake.


Amechakaza ngozi yangu na nyama yangu; Ameivunja mifupa yangu.


Naam, nikilia na kuomba msaada, Huyapinga maombi yangu.


Wala hawakunililia kwa moyo, lakini wanalalamika vitandani mwao; hujikutanisha ili kupata nafaka na divai; huniasi mimi.


Kisha wakaitwaa mifupa yao, na kuizika chini ya mkwaju huko Yabeshi, nao wakafunga siku saba.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo