Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Zaburi 32:10 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

10 Naye mtu mwovu ana mapigo mengi, Bali amtumainiaye BWANA fadhili zitamzunguka.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

10 Watu waovu watapata mateso mengi, bali wanaomtumainia Mwenyezi-Mungu wazungukwa na fadhili zake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

10 Watu waovu watapata mateso mengi, bali wanaomtumainia Mwenyezi-Mungu wazungukwa na fadhili zake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

10 Watu waovu watapata mateso mengi, bali wanaomtumainia Mwenyezi-Mungu wazungukwa na fadhili zake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

10 Mtu mwovu ana taabu nyingi, bali upendo usio na kikomo wa Mwenyezi Mungu unamzunguka mtu anayemtumaini.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

10 Mtu mwovu ana taabu nyingi, bali upendo usio na kikomo wa bwana unamzunguka mtu anayemtumaini.

Tazama sura Nakili




Zaburi 32:10
20 Marejeleo ya Msalaba  

Awanyeshee wasio haki mitego, Moto na kiberiti na upepo wa joto Na viwe fungu la kikombe chao.


Msingiziaji hatawekwa imara katika nchi, Mtu wa jeuri, uovu humwinda kumwangamiza.


Heri ambaye Mungu wa Yakobo ni msaada wake, Na tumaini lake ni kwa BWANA, Mungu wake,


BWANA huwaridhia wao wamchao, Na kuzitarajia fadhili zake.


Huzuni zao zitaongezeka Wambadilio Mungu kwa mwingine; Sitazimimina sadaka zao za damu, Wala kuyataja majina yao midomoni mwangu.


Shikeni yaliyo bora, asije akafanya hasira Nanyi mkapotea njiani, Kwa kuwa hasira yake huwaka upesi; Heri wote wanaomkimbilia.


Onjeni muone ya kuwa BWANA yu mwema; Heri mtu yule anayemtumainia.


Heri aliyemfanya BWANA kuwa tumaini lake, Wala hakuwaelekea wenye kiburi, Wala hao wanaogeukia uongo.


Kwa maana Wewe utambariki mwenye haki; BWANA, utamzungushia radhi kama ngao.


Ee BWANA wa majeshi, Heri mwanadamu anayekutumaini Wewe.


Uovu huwafuatia wenye dhambi; Bali mwenye haki atalipwa mema.


Atakayelitafakari neno atapata mema; Na kila amwaminiye BWANA ana heri.


Ijapokuwa mwenye dhambi amefanya maovu mara mia na akazidisha siku zake; lakini hata hivyo najua hakika ya kwamba itakuwa heri kwao wamchao Mungu, wenye kicho mbele zake;


Ole wake mtu mbaya; shari itakuwa kwake, kwa maana atapewa malipo ya mikono yake.


Hapana amani kwa waovu; asema Mungu wangu.


Maana shina moja la mabaya ya kila namna ni kupenda fedha; ambayo wengine hali wakiitamani hiyo wamefarakana na Imani, na kujichoma kwa maumivu mengi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo