Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Zaburi 31:5 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

5 Mikononi mwako naiweka roho yangu; Umenikomboa, Ee BWANA, Mungu wa kweli.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

5 Mikononi mwako naiweka roho yangu; umenikomboa, ee Mwenyezi-Mungu, Mungu mwaminifu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

5 Mikononi mwako naiweka roho yangu; umenikomboa, ee Mwenyezi-Mungu, Mungu mwaminifu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

5 Mikononi mwako naiweka roho yangu; umenikomboa, ee Mwenyezi-Mungu, Mungu mwaminifu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

5 Ninaikabidhi roho yangu mikononi mwako, unikomboe Ee Mwenyezi Mungu, uliye Mungu wa kweli.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

5 Ninaikabidhi roho yangu mikononi mwako, unikomboe Ee bwana, uliye Mungu wa kweli.

Tazama sura Nakili




Zaburi 31:5
15 Marejeleo ya Msalaba  

naye Malaika aliyeniokoa na maovu yote, na awabariki vijana hawa; jina langu na litajwe juu yao, na jina la baba zangu, Abrahamu na Isaka; na wawe wingi wa watu kati ya nchi.


Yeye atamkomboa Israeli na maovu yake yote.


Midomo yangu itafurahi sana nikuimbiapo, Na nafsi yangu uliyoikomboa.


Basi, nilipokuja, mbona hapakuwa na mtu? Nilipoita, mbona hapakuwa na mtu aliyenijibu? Je! Mkono wangu ni mfupi, hata nisiweze kukomboa? Au je! Mimi sina nguvu za kuponya? Tazama, kwa kukemea kwangu naikausha bahari, mito ya maji naifanya kuwa jangwa; samaki wao wanuka kwa sababu hapana maji, nao wafa kwa kiu.


baada ya kuuzwa aweza kukombolewa; mtu mmoja miongoni mwa ndugu zake ana ruhusa kumkomboa;


Yesu akalia kwa sauti kuu, akasema, Ee Baba, mikononi mwako naiweka roho yangu.


Wakampiga kwa mawe Stefano, naye akiomba, akisema, Bwana Yesu, pokea roho yangu.


Yeye Mwamba, kazi yake ni kamilifu; Maana, njia zake zote ni haki. Mungu wa uaminifu, asiye na uovu, Yeye ndiye mwenye haki na adili.


Kwa sababu hiyo nimepatikana na mateso haya, lakini sitahayari; kwa maana namjua yeye niliyemwamini, na kusadiki ya kwamba aweza kukilinda kile nilichokiweka amana kwake hata siku ile.


Kama sisi hatuamini, yeye hudumu wa kuaminiwa. Kwa maana hawezi kujikana mwenyewe.


katika tumaini la uzima wa milele, ambao Mungu asiyeweza kusema uongo aliuahidi tangu milele;


ambaye alijitoa nafsi yake kwa ajili yetu, ili atukomboe na maasi yote, na kujisafishia watu wake mwenyewe walio na bidii katika matendo mema.


ili kwa vitu viwili visivyoweza kubadilika, ambavyo katika hivyo Mungu hawezi kusema uongo, tupate faraja iliyo imara, sisi tuliokimbilia kuyashika matumaini yale yawekwayo mbele yetu;


Nao waimba wimbo mpya wakisema, Wastahili wewe kukitwaa hicho kitabu na kuifungua mihuri yake; kwa kuwa ulichinjwa, ukawa fidia kwa Mungu na kwa damu yako watu wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa,


Tufuate:

Matangazo


Matangazo