Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Zaburi 31:23 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

23 Mpendeni BWANA, Ninyi nyote mlio watauwa wake. BWANA huwahifadhi waaminifu, Bali humlipiza mwenye kiburi ipasavyo.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

23 Mpendeni Mwenyezi-Mungu, enyi watakatifu wake wote. Mwenyezi-Mungu huwalinda watu waaminifu; lakini huwaadhibu kabisa wenye kiburi wanavyostahili.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

23 Mpendeni Mwenyezi-Mungu, enyi watakatifu wake wote. Mwenyezi-Mungu huwalinda watu waaminifu; lakini huwaadhibu kabisa wenye kiburi wanavyostahili.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

23 Mpendeni Mwenyezi-Mungu, enyi watakatifu wake wote. Mwenyezi-Mungu huwalinda watu waaminifu; lakini huwaadhibu kabisa wenye kiburi wanavyostahili.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

23 Mpendeni Mwenyezi Mungu ninyi watakatifu wake wote! Mwenyezi Mungu huwahifadhi waaminifu, lakini wenye kiburi huwalipiza kikamilifu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

23 Mpendeni bwana ninyi watakatifu wake wote! bwana huwahifadhi waaminifu, lakini wenye kiburi huwalipiza kikamilifu.

Tazama sura Nakili




Zaburi 31:23
22 Marejeleo ya Msalaba  

Ee BWANA, kazi zako zote zitakushukuru, Na wacha Mungu wako watakuhimidi.


BWANA huwahifadhi wote wampendao, Na wote wasio haki atawaangamiza.


Mwimbieni BWANA zaburi, Enyi watauwa wake. Na kutoa shukrani. Kwa kukumbuka utakatifu wake.


Mcheni BWANA, enyi watakatifu wake, Maana, wamchao hawapungukiwi kitu.


Atawarudishia adui zangu ubaya wao; Uwaangamize kwa uaminifu wako.


Mungu huogopwa sana barazani pa watakatifu, Ni wa kuhofiwa kuliko wote wanaomzunguka.


Mwenye kuihukumu nchi, ujitukuze, Uwape wenye kiburi stahili zao.


Enyi mmpendao BWANA, uchukieni uovu; Huwalinda nafsi zao watauwa wake, Na kuwaokoa na mkono wa wasio haki.


Nilisema, Katika usitawi wa siku zangu nitakwenda kuingia malango ya kuzimu; Nimenyimwa mabaki ya miaka yangu.


Na wageni, walioandamana na BWANA ili wamhudumu, na kulipenda jina la BWANA, kuwa watumishi wake; kila aishikaye sabato asiivunje, na kulishika sana agano langu;


Kisha akaniambia, Mwanadamu, mifupa hii ni nyumba yote ya Israeli; tazama, wao husema, Mifupa yetu imekauka, matumaini yetu yametupotea; tumekatiliwa mbali kabisa.


Basi, katika kiyama atakuwa mke wa yupi katika hao? Maana wote saba walikuwa naye.


Na sasa, Israeli, BWANA, Mungu wako, anataka nini kwako, ila umche BWANA, Mungu wako, na kwenda katika njia zake zote, na kumpenda, na kumtumikia BWANA, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote;


kwa hivi nikuagizavyo leo kumpenda BWANA, Mungu wako, kuenenda katika njia zake, na kushika maagizo yake, na amri zake, na hukumu zake, upate kuwa hai na kuongezeka; BWANA, Mungu wako, apate kukubarikia katika nchi uingiayo kuimiliki.


Nikiunoa upanga wangu wa umeme, Mkono wangu ukishika hukumu, Nitawatoza kisasi adui zangu, Nitawalipa wanaonichukia.


Hakika awapenda hayo makabila ya watu; Watakatifu wake wote wamo mkononi mwako; Nao waliketi miguuni pako; Watapokea kila mmoja katika maneno yako.


Iliyobaki, ndugu, tunawasihi na kuwaonya kwamba mwenende katika Bwana Yesu; kama mlivyopokea kwetu jinsi iwapasavyo kuenenda na kumpendeza Mungu, kama nanyi mnavyoenenda, vivyo hivyo mpate kuzidi sana.


Yuda, mtumwa wa Yesu Kristo, ndugu yake Yakobo, kwa hao walioitwa, waliopendwa katika Mungu Baba, na kuhifadhiwa kwa ajili ya Yesu Kristo.


Mlipeni kama yeye alivyolipa, mkamlipe mara mbili kwa kadiri ya matendo yake. Katika kikombe kile alichokichanganyisha, mchanganyishieni mara mbili.


Yeye atailinda miguu ya watakatifu wake; Bali waovu watanyamazishwa gizani, Maana kwa nguvu hakuna atakayeshinda;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo