Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Zaburi 31:17 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

17 Ee BWANA, nisiaibishwe, maana nimekuita; Waaibishwe wasio haki, wanyamaze kuzimuni.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

17 Usiniache niaibike ee Mwenyezi-Mungu, maana mimi ninakuomba; lakini waache waovu waaibike, waache wapotelee kwa mshangao huko kuzimu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

17 Usiniache niaibike ee Mwenyezi-Mungu, maana mimi ninakuomba; lakini waache waovu waaibike, waache wapotelee kwa mshangao huko kuzimu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

17 Usiniache niaibike ee Mwenyezi-Mungu, maana mimi ninakuomba; lakini waache waovu waaibike, waache wapotelee kwa mshangao huko kuzimu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

17 Usiniache niaibike, Ee Mwenyezi Mungu, kwa maana nimekulilia wewe, bali waovu waaibishwe na kunyamazishwa Kuzimu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

17 Usiniache niaibike, Ee bwana, kwa maana nimekulilia wewe, bali waovu waaibishwe na kunyamazishwa Kuzimu.

Tazama sura Nakili




Zaburi 31:17
25 Marejeleo ya Msalaba  

Wafu hawamsifu Mungu BWANA, Wala yeyote ashukaye kwenye kimya;


Nimekukimbilia Wewe, BWANA, Nisiaibike milele. Kwa haki yako uniponye,


Mwelekezeeni macho, mpate kufurahi, Na nyuso zenu hazitaaibishwa kamwe.


Waaibishwe, wafedheheshwe pamoja, Wanaoifurahia hali yangu mbaya. Wavikwe aibu na fedheha, Wanaojikuza juu yangu.


Waaibike na kufedheheka, Wanaoitafuta nafsi yangu. Warudishwe nyuma, wafadhaishwe, Wanaonizulia mabaya.


Umenitia furaha moyoni mwangu, Kupita yao wanapozidishiwa nafaka na divai.


Adui zangu wote wataaibika na kufadhaika, Watarudi nyuma, kwa ghafla wataaibika.


Ulimi wangu nao utasimulia Haki yako mchana kutwa. Kwa maana wameaibishwa, Wametahayarika, wanaonitakia mabaya.


Ee BWANA, Mungu wa majeshi, hadi lini Utayaghadhibikia maombi ya watu wako?


Ulileta mzabibu kutoka Misri, Ukawafukuza mataifa ukaupanda.


Kama BWANA asingalikuwa msaada wangu, Nafsi yangu kwa upesi ingalikaa penye kimya.


Lakini BWANA yuko pamoja nami, mfano wa shujaa mwenye kutisha; kwa hiyo hao wanaonionea watajikwaa, wala hawatashinda; watatahayarika sana. Kwa sababu hawatafaulu wataona aibu ya milele, ambayo haitasahauliwa kamwe.


Tena, wengi wa hao wanaolala katika mavumbi ya nchi wataamka, wengine wapate uzima wa milele, wengine aibu na kudharauliwa milele.


Yeye atailinda miguu ya watakatifu wake; Bali waovu watanyamazishwa gizani, Maana kwa nguvu hakuna atakayeshinda;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo