Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Zaburi 30:12 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

12 Ili nafsi yangu ikusifu, Wala isinyamaze. Ee BWANA, Mungu wangu, Nitakushukuru milele.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

12 Mimi nitakusifu wala sitakaa kimya. Ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu nitakushukuru milele.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

12 Mimi nitakusifu wala sitakaa kimya. Ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu nitakushukuru milele.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

12 Mimi nitakusifu wala sitakaa kimya. Ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu nitakushukuru milele.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

12 ili moyo wangu uweze kukusifu na usikae kimya. Ee Mwenyezi Mungu, Mungu wangu, nitakushukuru milele.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

12 ili moyo wangu uweze kukusifu na usikae kimya. Ee bwana Mwenyezi Mungu wangu, nitakushukuru milele.

Tazama sura Nakili




Zaburi 30:12
16 Marejeleo ya Msalaba  

Nafsi yangu, usiingie katika siri yao, Fahari yangu usiungane na kusanyiko lao, Maana katika ghadhabu yao walimwua mtu, Na kwa ukaidi wao walikata mshipa wa ng'ombe;


Ikawa nuru na furaha na shangwe na heshima kwa Wayahudi.


siku ambazo Wayahudi walijipatia raha mbele ya adui zao, na mwezi uliogeuzwa kwao kuwa furaha badala ya huzuni, na kuwa sikukuu badala ya kilio; wazifanye siku hizo ziwe za karamu na furaha, za kupeana zawadi na za kuwapa maskini tunu.


Naam, nitamwimbia BWANA, Kwa kuwa amenitendea kwa ukarimu.


Kila siku nitakuhimidi, Nitalisifu jina lako milele na milele.


Kwa hiyo moyo wangu unafurahi, Nayo nafsi yangu inashangilia, Naam, mwili wangu nao utakaa kwa kutumaini.


Tumejisifia Mungu mchana kutwa, Na jina lako tutalishukuru milele.


Amka, ee moyo wangu. Amka, kinanda na kinubi, Nitaamka alfajiri.


Lakini mimi nitakutumainia daima, Nitaendelea kukusifu zaidi na zaidi.


Midomo yangu itafurahi sana nikuimbiapo, Na nafsi yangu uliyoikomboa.


kuwaagizia hao waliao katika Sayuni, wapewe taji la maua badala ya majivu, mafuta ya furaha badala ya maombolezo, vazi la sifa badala ya roho nzito; wapate kuitwa miti ya haki, iliyopandwa na BWANA, ili atukuzwe.


Akajibu, akasema, Nawaambia ninyi, wakinyamaza hawa, mawe yatanena kwa sauti kuu.


maana sisi hatuwezi kuacha kuyanena mambo tuliyoyaona na kuyasikia.


wakisema, Amina; Baraka na utukufu na hekima na shukrani na heshima na uweza na nguvu zina Mungu wetu hata milele na milele. Amina.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo