Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Zaburi 3:4 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

4 Kwa sauti yangu namwita BWANA Naye aniitikia toka mlima wake mtakatifu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

4 Nakulilia kwa sauti, ee Mungu, nawe wanisikiliza kutoka mlima wako mtakatifu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

4 Nakulilia kwa sauti, ee Mungu, nawe wanisikiliza kutoka mlima wako mtakatifu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

4 Nakulilia kwa sauti, ee Mungu, nawe wanisikiliza kutoka mlima wako mtakatifu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

4 Ninamlilia Mwenyezi Mungu kwa sauti kuu, naye ananijibu kutoka mlima wake mtakatifu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

4 Ninamlilia bwana kwa sauti kuu, naye ananijibu kutoka mlima wake mtakatifu.

Tazama sura Nakili




Zaburi 3:4
29 Marejeleo ya Msalaba  

Baada ya mambo hayo neno la BWANA likamjia Abramu katika njozi, likinena, Usiogope, Abramu, Mimi ni ngao yako, na thawabu yako itakuwa kubwa sana.


Ndiwe sitara yangu na ngao yangu, Neno lako nimelingojea.


Siku ile niliyokuita uliniitikia, Ukanifariji nafsi kwa kunitia nguvu.


Namwita BWANA astahiliye kusifiwa, Hivyo nitaokoka na adui zangu.


Nami nimemweka mfalme wangu Juu ya Sayuni, mlima wangu mtakatifu.


Na sasa kichwa changu kitainuka Juu ya adui zangu wanaonizunguka. Nami nitatoa dhabihu za shangwe hemani mwake; Nitaimba, naam, nitamhimidi BWANA.


BWANA ni nguvu zangu na ngao yangu. Moyo wangu umemtumaini, Nami nimesaidiwa; Basi, moyo wangu unashangilia, Na kwa wimbo wangu nitamshukuru.


Nilimtafuta BWANA, naye akanijibu, Akaniokoa kutoka kwa hofu zangu zote.


Maskini huyu aliita, BWANA akasikia, Akamwokoa na taabu zake zote.


Nitumie nuru yako na kweli yako ziniongoze, Zinifikishe kwenye mlima wako mtakatifu na hata katika maskani yako.


Uniite siku ya mateso; Nitakuokoa, nawe utanitukuza.


Enyi watu, mtumainini sikuzote, Ifunueni mioyo yenu mbele zake; Mungu ndiye kimbilio letu.


Ee BWANA wa majeshi, Heri mwanadamu anayekutumaini Wewe.


Ndipo ulipowaambia watakatifu wako kwa maono, Ukasema, Nimempa aliye hodari msaada; Nimemtukuza aliyechaguliwa miongoni mwa watu.


Ataniita nami nitamwitikia; Nitakuwa pamoja naye taabuni, Nitamwokoa na kumtukuza;


Mtukuzeni BWANA, Mungu wetu; Sujuduni mkiukabili mlima wake mtakatifu; Maana BWANA, Mungu wetu, ni mtakatifu.


Huwawekea wanyofu akiba ya hekima kamili; Yeye ni ngao kwao waendao kwa ukamilifu;


Na itakuwa ya kwamba, kabla hawajaomba, nitajibu; na wakiwa bado wanena, nitasikia.


Ukaisikia sauti yangu; usifiche sikio lako Ili usisikie pumzi yangu, kwa kilio changu.


Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa;


Kuna mtu miongoni mwenu anayeteseka? Na aombe. Ana moyo wa kuchangamka? Na aimbe zaburi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo