Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Zaburi 29:10 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

10 BWANA aketi juu ya Gharika; Naam, BWANA ameshika hatamu ya ufalme milele.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

10 Mwenyezi-Mungu ameketi juu ya gharika; Mwenyezi-Mungu ni mfalme atawalaye milele.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

10 Mwenyezi-Mungu ameketi juu ya gharika; Mwenyezi-Mungu ni mfalme atawalaye milele.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

10 Mwenyezi-Mungu ameketi juu ya gharika; Mwenyezi-Mungu ni mfalme atawalaye milele.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

10 Mwenyezi Mungu huketi akiwa ametawazwa juu ya gharika; Mwenyezi Mungu ametawazwa kuwa Mfalme milele.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

10 bwana huketi akiwa ametawazwa juu ya gharika; bwana ametawazwa kuwa Mfalme milele.

Tazama sura Nakili




Zaburi 29:10
16 Marejeleo ya Msalaba  

Tazama, nitaleta gharika ya maji juu ya nchi, niharibu kila kitu chenye mwili na pumzi ya uhai, kisiwepo chini ya mbingu; kila kilichoko duniani kitakufa.


Ni nani aliyepasua mfereji kwa maji ya gharika, Au njia kwa umeme wa radi;


BWANA ndiye Mfalme milele na milele; Mataifa yataangamia kutoka nchi yake.


Sauti ya BWANA inasikika juu ya maji; Mungu wa utukufu apiga radi; BWANA yu juu ya maji mengi.


Watuliza kuvuma kwa bahari, Kuvuma kwa mawimbi yake, Na ghasia za watu;


Naye atauhukumu ulimwengu kwa haki; Atawaamua watu kwa uadilifu.


BWANA ametamalaki, amejivika adhama, BWANA amejivika, ukuu na nguvu, kama mavazi ya kifalme. Naam, ulimwengu umethibitika usitikisike;


BWANA ametamalaki, mataifa wanatetemeka; Ameketi juu ya makerubi, nchi inatikisika.


Na katika siku za wafalme hao Mungu wa mbinguni atausimamisha ufalme ambao hautaangamizwa milele, wala watu wengine hawataachiwa enzi yake; bali utavunja falme hizi zote vipande vipande na kuziharibu, nao utasimama milele na milele.


Na usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu. [Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele. Amina.]


Wakaingiwa na hofu kuu, wakaambiana, Ni nani huyu, basi, hata upepo na bahari humtii?


Sasa kwa Mfalme wa milele, asiyeweza kuona uharibifu, asiyeonekana, Mungu peke yake, na iwe heshima na utukufu milele na milele. Amina.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo