Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Zaburi 28:3 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

3 Usinikokote pamoja na wasio haki, Wala pamoja na watenda maovu. Wawaambiao jirani zao maneno ya amani, Lakini mioyoni mwao mna madhara.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

3 Usinipatilize pamoja na watu wabaya, pamoja na watu watendao maovu: Watu wasemao na wenzao maneno ya amani, kumbe wamejaa uhasama moyoni.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

3 Usinipatilize pamoja na watu wabaya, pamoja na watu watendao maovu: Watu wasemao na wenzao maneno ya amani, kumbe wamejaa uhasama moyoni.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

3 Usinipatilize pamoja na watu wabaya, pamoja na watu watendao maovu: watu wasemao na wenzao maneno ya amani, kumbe wamejaa uhasama moyoni.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

3 Usiniburute pamoja na waovu, pamoja na hao watendao mabaya, ambao huzungumza na majirani zao maneno mazuri, lakini mioyoni mwao wameficha chuki.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

3 Usiniburute pamoja na waovu, pamoja na hao watendao mabaya, ambao huzungumza na jirani zao maneno mazuri, lakini mioyoni mwao wameficha chuki.

Tazama sura Nakili




Zaburi 28:3
17 Marejeleo ya Msalaba  

Umeona, maana unaangalia matatizo na dhiki, Uyatwae mkononi mwako. Mtu duni hukuachia nafsi yake, Maana umekuwa msaidizi wa yatima.


Kinywa chake kimejaa laana, Na hila na dhuluma. Chini ya ulimi wake kuna madhara na uovu,


Husemezana yasiyofaa kila mtu na mwenziwe, Wenye midomo ya kujipendekeza; Husemezana kwa mioyo ya unafiki;


Usiuelekeze moyo wangu kunako jambo baya, Nisiyazoelee matendo yasiyofaa, Pamoja na watu watendao maovu; Wala nisile vyakula vyao vya anasa.


Usiiondoe nafsi yangu pamoja na wakosaji, Wala uhai wangu pamoja na wauaji.


Huwaza maovu kitandani pake, Hujiweka katika njia mbaya; hauchukii ubaya.


Kwa nini kujisifia uovu, Ewe jabari? Wema wa Mungu upo sikuzote.


Kinywa chake ni laini kuliko siagi, Bali moyo wake ni vita. Maneno yake ni mororo kuliko mafuta, Lakini yanakata kama upanga mkali.


Mpango wao ni kumwangusha tu mtu mwenye cheo; Huufurahia uongo. Kwa kinywa chao hubariki; Kwa moyo wao hulaani.


Tazama, huyu ametunga uovu, Amechukua mimba ya madhara, amezaa uongo.


BWANA asema hivi kuhusu manabii wanaowakosesha watu wangu; hao waumao kwa meno yao, na kulia, Amani; na mtu awaye yote asiyetia kitu vinywani mwao, wao humwandalia vita.


Akasema na mkutano, na kuwaambia, Nawasihi, ondokeni penye hema za hawa watu waovu, wala msiguse kitu chao chochote, msiangamizwe katika dhambi zao zote.


Kisha atawaambia na wale walioko katika mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake;


Na hao watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele; bali wenye haki watakwenda katika uzima wa milele.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo