Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Zaburi 28:1 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

1 Ee BWANA, nitakuita Ewe, mwamba wangu, Usiwe kwangu kama kiziwi. Nisije nikafanana nao washukao shimoni, Ikiwa umeninyamalia.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 Nakulilia, ee Mwenyezi-Mungu! Ewe mwamba wa usalama wangu usiniwie kama kiziwi, la sivyo kama usiponisikiliza, nitakuwa kama wale washukao shimoni kwa wafu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 Nakulilia, ee Mwenyezi-Mungu! Ewe mwamba wa usalama wangu usiniwie kama kiziwi, la sivyo kama usiponisikiliza, nitakuwa kama wale washukao shimoni kwa wafu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Nakulilia, ee Mwenyezi-Mungu! Ewe mwamba wa usalama wangu usiniwie kama kiziwi, la sivyo kama usiponisikiliza, nitakuwa kama wale washukao shimoni kwa wafu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Ninakuita wewe, Ee Mwenyezi Mungu, Mwamba wangu; usikatae kunisikiliza. Kwa sababu ukinyamaza nitafanana na walioshuka shimoni.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Ninakuita wewe, Ee bwana, Mwamba wangu; usiwe kwangu kama kiziwi. Kwa sababu ukinyamaza nitafanana na walioshuka shimoni.

Tazama sura Nakili




Zaburi 28:1
21 Marejeleo ya Msalaba  

Yeye ameikomboa nafsi yangu isiende shimoni, Na uhai wangu utautazama mwanga.


Kwa sauti yangu nitamlilia BWANA, Kwa sauti yangu nitamwomba BWANA dua.


Nitafunua mbele zake malalamiko yangu, Shida yangu nitaitangaza mbele zake.


Ee BWANA, unijibu hima, roho yangu imelegea; Usinifiche uso wako, Nisifanane nao washukao shimoni.


BWANA ni jabali langu, na boma langu, na mwokozi wangu, Mungu wangu, mwamba wangu ninayemkimbilia, Ngao yangu, na pembe ya wokovu wangu, na ngome yangu.


Ee Mungu wangu, nalia mchana lakini hujibu Na wakati wa usiku lakini sipati raha.


Kwa sauti yangu namwita BWANA Naye aniitikia toka mlima wake mtakatifu.


Mwimbieni BWANA zaburi, Enyi watauwa wake. Na kutoa shukrani. Kwa kukumbuka utakatifu wake.


Mna faida gani katika damu yangu Nishukapo Shimoni? Mavumbi yatakusifu? Yatautangaza uaminifu wako?


Wewe, BWANA, umeona, usinyamaze; Ee Bwana, usiwe mbali nami.


Ee BWANA, usikie maombi yangu, Utege sikio lako niliapo, Usiyapuuze machozi yangu. Kwa maana mimi ni mgeni wako, Msafiri kama baba zangu wote.


Nitamwambia Mungu, mwamba wangu, Kwa nini umenisahau? Kwa nini ninakwenda nikihuzunika, adui wakinionea?


Uisikie sauti ya kilio changu, Ee Mfalme wangu na Mungu wangu, Kwa maana Wewe ndiwe nikuombaye.


Mkondo usinigharikishe, wala vilindi visinimeze, Wala Shimo lisifumbe kinywa chake juu yangu.


Nimpazie Mungu sauti yangu, Naam, nimpazie Mungu, naye atanisikia.


Ee Mungu, usistarehe, Ee Mungu, usinyamae, wala usitulie.


Tuwameze hai kama kuzimu, Na wazima, kama wao washukao shimoni.


Mtumainini BWANA siku zote Maana BWANA YEHOVA ni mwamba wa milele.


Kwa kuwa kuzimu hakuwezi kukusifu; mauti haiwezi kukuadhimisha; Wale washukao shimoni hawawezi kuutumainia uaminifu wako.


akamtupa katika kuzimu, akamfunga, akatia mhuri juu yake, asipate kuwadanganya mataifa tena, hata ile miaka elfu itimie; na baada ya hayo yapasa afunguliwe kwa muda mfupi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo