Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Zaburi 21:3 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

3 Maana umemsogezea baraka za heri, Umemvika taji la dhahabu safi kichwani pake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

3 Umemjia, ukampa baraka nzurinzuri; umemvika taji ya dhahabu safi kichwani mwake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

3 Umemjia, ukampa baraka nzurinzuri; umemvika taji ya dhahabu safi kichwani mwake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

3 Umemjia, ukampa baraka nzurinzuri; umemvika taji ya dhahabu safi kichwani mwake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

3 Ulimkaribisha kwa baraka tele na kumvika taji la dhahabu safi kichwani pake.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

3 Ulimkaribisha kwa baraka tele na kumvika taji ya dhahabu safi kichwani pake.

Tazama sura Nakili




Zaburi 21:3
16 Marejeleo ya Msalaba  

Kisha akamnyang'anya mfalme wao taji toka kichwani pake; na uzani wake ulikuwa talanta ya dhahabu, nalo lilikuwa na vito vya thamani ndani yake; akavikwa Daudi kichwani. Akazitoa nyara za huo mji, nyingi sana.


Basi watu wa Yuda wakaenda, wakamtia Daudi mafuta huko, awe mfalme juu ya nyumba ya Yuda. Wakamwambia Daudi wakasema, Watu wa Yabesh-gileadi ndio waliomzika Sauli.


Basi wazee wote wa Israeli wakamwendea mfalme huko Hebroni, naye mfalme Daudi akapatana nao huko Hebroni mbele za BWANA; wakamtia Daudi mafuta awe mfalme juu ya Israeli.


Kisha Daudi akatwaa taji la Milkomu toka kichwani pake, akaona ya kwamba uzani wake ni talanta ya dhahabu, na kulikuwa na vito vya thamani ndani yake; akavikwa Daudi kichwani; akazitoa nyara za mji, nyingi sana.


Sasa, Ee BWANA, Mungu, uondoke, uende kwenye raha yako, wewe na sanduku la nguvu zako; makuhani wako, Ee BWANA, Mungu, wavikwe wokovu, watakatifu wako na washangilie mema.


Ni nani aliyetangulia kunipa hata nimlipe? Kila kilicho chini ya mbingu nzima ni changu.


Walinikabili siku ya msiba wangu, Lakini BWANA alikuwa tegemeo langu.


Na tuushangilie wokovu wako, Kwa jina la Mungu wetu tuzitweke bendera zetu. BWANA akutimizie matakwa yako yote.


Jinsi zilivyo nyingi fadhili zako Ulizowawekea wakuchao; Ulizowatendea wakukimbiliao Mbele ya wanadamu!


Mungu wa fadhili zangu atanitangulia, Mungu atanijalia kutazama kwa ushindi juu ya adui zangu.


Au ni nani aliyempa yeye kitu kwanza, naye atalipwa tena?


Au waudharau wingi wa wema wake na ustahimili wake na uvumilivu wake, usijue ya kuwa wema wa Mungu wakuvuta upate kutubu?


Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo;


ila twamwona yeye aliyefanywa mdogo kwa muda kuliko malaika, yaani, Yesu, kwa sababu ya maumivu ya mauti, amevikwa taji la utukufu na heshima, ili kwa neema ya Mungu aionje mauti kwa ajili ya kila mtu.


Na macho yake yalikuwa kama muali wa moto, na juu ya kichwa chake vilemba vingi; naye ana jina lililoandikwa, asilolijua mtu ila yeye mwenyewe.


Ndipo Samweli akaitwaa pembe yenye mafuta, akamtia mafuta kati ya ndugu zake; na Roho ya BWANA ikamjia Daudi kwa nguvu kuanzia siku ile. Basi Samweli akaondoka, akaenda zake Rama.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo