Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Zaburi 20:5 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

5 Na tuushangilie wokovu wako, Kwa jina la Mungu wetu tuzitweke bendera zetu. BWANA akutimizie matakwa yako yote.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

5 Tutashangilia kwa ajili ya ushindi wako; tutatweka bendera kulitukuza jina la Mungu wetu. Mwenyezi-Mungu akutimizie maombi yako yote!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

5 Tutashangilia kwa ajili ya ushindi wako; tutatweka bendera kulitukuza jina la Mungu wetu. Mwenyezi-Mungu akutimizie maombi yako yote!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

5 Tutashangilia kwa ajili ya ushindi wako; tutatweka bendera kulitukuza jina la Mungu wetu. Mwenyezi-Mungu akutimizie maombi yako yote!

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

5 Tutashangilia kwa furaha utakaposhinda, tutainua bendera zetu kwa jina la Mungu wetu. Mwenyezi Mungu na akupe haja zako zote.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

5 Tutashangilia kwa furaha utakaposhinda, tutainua bendera zetu kwa jina la Mungu wetu. bwana na akupe haja zako zote.

Tazama sura Nakili




Zaburi 20:5
19 Marejeleo ya Msalaba  

Sauti ya furaha na wokovu Imo hemani mwao wenye haki; Mkono wa kulia wa BWANA hutenda makuu.


Lakini mimi nimezitumainia fadhili zako; Moyo wangu na uufurahie wokovu wako.


Sauti yao imeenea duniani kote, Na maneno yao hadi miisho ya ulimwengu. Katika hizo ameliwekea jua hema,


Ee BWANA, mfalme atazifurahia nguvu zako, Na wokovu wako ataufanyia shangwe nyingi sana.


Maana umemsogezea baraka za heri, Umemvika taji la dhahabu safi kichwani pake.


Na nafsi yangu itamfurahia BWANA, Na kuushangilia wokovu wake.


Umewapa wakuogopao bendera, Ili itwekwe kwa ajili ya kweli.


Ili nizisimulie sifa zako zote; Katika malango ya binti Sayuni Nitaufurahia wokovu wako.


Musa akajenga madhabahu, akaiita jina lake Yahweh-nisi;


Na itakuwa katika siku hiyo, shina la Yese lisimamalo kuwa ishara kwa makabila ya watu, yeye ndiye ambaye mataifa watamtafuta; na mahali pake pa kupumzikia patakuwa na utukufu.


Katika siku hiyo watasema, Tazama, huyu ndiye Mungu wetu, Ndiye tuliyemngoja atusaidie; Huyu ndiye BWANA tuliyemngoja, Na tushangilie na kuufurahia wokovu wake.


Nitafurahi sana katika BWANA, nafsi yangu itashangilia katika Mungu wangu; maana amenivika mavazi ya wokovu, amenifunika vazi la haki, kama bwana arusi ajipambavyo kwa kilemba cha maua, na kama bibi arusi ajipambavyo kwa vyombo vya dhahabu.


Kwa maana mataifa yote watakwenda, kila moja kwa jina la mungu wake, na sisi tutakwenda kwa jina la BWANA, Mungu wetu, milele na milele.


Walakini nitamfurahia BWANA Nitamshangilia Mungu wa wokovu wangu.


Na roho yangu imemfurahia Mungu, Mwokozi wangu;


Ndipo Eli akajibu, akasema, Nenda kwa amani; na Mungu wa Israeli akujalie haja yako uliyomwomba.


Ndipo Daudi akamwambia yule Mfilisti, Wewe unanijia mimi na upanga, na fumo, na mkuki, bali mimi ninakujia wewe kwa jina la BWANA wa majeshi, Mungu wa majeshi ya Israeli uliowatukana.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo