Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Zaburi 18:8 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

8 Kukapanda moshi kutoka puani mwake, Moto wa kuteketeza ukatoka kinywani mwake, Makaa ya moto yakamtoka.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

8 Moshi ulifuka kutoka puani mwake, moto uunguzao ukatoka kinywani mwake; makaa ya moto yalilipuka kutoka kwake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

8 Moshi ulifuka kutoka puani mwake, moto uunguzao ukatoka kinywani mwake; makaa ya moto yalilipuka kutoka kwake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

8 Moshi ulifuka kutoka puani mwake, moto uunguzao ukatoka kinywani mwake; makaa ya moto yalilipuka kutoka kwake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

8 Moshi ukapanda kutoka puani mwake, moto uteketezao ukatoka kinywani mwake, makaa ya moto yanayowaka yakatoka ndani yake.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

8 Moshi ukapanda kutoka puani mwake, moto uteketezao ukatoka kinywani mwake, makaa ya moto yawakayo yakatoka ndani mwake.

Tazama sura Nakili




Zaburi 18:8
18 Marejeleo ya Msalaba  

naye akatazama upande wa Sodoma na Gomora na nchi yote ya hilo Bonde, akaona, na tazama, moshi wa nchi ukapanda, kama moshi wa tanuri.


Mienge iwakayo hutoka kinywani mwake, Na cheche za moto huruka nje.


Aitazamaye nchi, ikatetemeka; Aigusaye milima, ikatoka moshi.


Awanyeshee wasio haki mitego, Moto na kiberiti na upepo wa joto Na viwe fungu la kikombe chao.


Utawafanya kuwa kama tanuri ya moto, Wakati wa ghadhabu yako. BWANA atawameza kwa ghadhabu yake, Na moto utawateketeza.


Mungu wetu atakuja wala sio kimya kimya, Moto utakula mbele zake, na tufani yavuma sana ikimzunguka pande zote.


Ee Mungu, mbona umetutupa milele? Kwa nini hasira yako inatoka moshi Juu ya kondoo wa malisho yako?


Itakuwa kila akimbiaye sauti ya hofu ataanguka katika shimo; na kila apandaye na kutoka shimoni atanaswa na mtego; kwa maana madirisha yaliyo juu yamewekwa wazi, na misingi ya dunia inatikisika.


Mto kama wa moto ukatoka ukapita mbele zake; maelfu wakamtumikia, na mamilioni wakasimama mbele zake; hukumu ikawekwa, na vitabu vikafunuliwa.


Kisha moto ukatoka hapo mbele za BWANA, na ukawateketeza, nao wakafa mbele za BWANA.


Baadhi yenu nimewaangamiza, kama hapo Mungu alipoiangamiza Sodoma na Gomora, nanyi mkawa kama kinga kilichonyakuliwa motoni; lakini hamkunirudia mimi, asema BWANA.


Kisha hao watu walikuwa kama wanung'unikao, wakinena maovu masikioni mwa BWANA; BWANA aliposikia hayo, hasira zake zikawaka; na moto wa BWANA ukawaka kati yao, ukateketeza hadi viunga vya kambi.


Kisha moto ukatoka kwa BWANA, ukawateketeza hao watu mia mbili hamsini waliofukiza uvumba.


BWANA hatamsamehe mtu huyo, lakini wakati huo hasira ya BWANA na wivu wake vitafuka moshi juu ya mtu yule, na laana yote iliyoandikwa katika kitabu hiki itamkalia juu yake, na BWANA atalifuta jina lake chini ya mbingu.


Na mtu akitaka kuwadhuru, moto hutoka katika vinywa vyao na kuwala adui zao. Na mtu akitaka kuwadhuru, hivyo ndivyo impasavyo kuuawa.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo