Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Zaburi 18:7 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

7 Ndipo nchi iliyotikisika na kutetemeka, Misingi ya milima ikatingizika; Ikatikisika kwa sababu alikuwa na ghadhabu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

7 Hapo dunia ikatetemeka na kutikisika; misingi ya milima ikayumbayumba, kwani Mungu alikuwa amekasirika.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

7 Hapo dunia ikatetemeka na kutikisika; misingi ya milima ikayumbayumba, kwani Mungu alikuwa amekasirika.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

7 Hapo dunia ikatetemeka na kutikisika; misingi ya milima ikayumbayumba, kwani Mungu alikuwa amekasirika.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

7 Dunia ilitetemeka na kutikisika, misingi ya milima ikatikisika; vilitetemeka kwa sababu alikuwa amekasirika.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

7 Dunia ilitetemeka na kutikisika, misingi ya milima ikatikisika, vilitetemeka kwa sababu alikuwa amekasirika.

Tazama sura Nakili




Zaburi 18:7
18 Marejeleo ya Msalaba  

Uso wa BWANA ni juu ya watenda mabaya, Aliondoe kumbukumbu lao duniani.


BWANA yu karibu nao waliovunjika moyo, Na huwaokoa waliopondeka roho.


Uache kunitazama, ndio nipate kufurahi tena, Kabla sijafa na kutoweka kabisa.


Akanipandisha toka shimo la uharibifu, Toka udongo wa utelezi; Akaisimamisha miguu yangu mwambani, Akaziimarisha hatua zangu.


Kwa hiyo hatutaogopa ijapobadilika nchi, Ijapotetemeka milima moyoni mwa bahari.


Niliiangalia milima, na tazama, ilitetemeka, na milima yote ilisogea huku na huko.


Milima ilikuona, ikaogopa; Gharika ya maji ikapita; Vilindi vikatoa sauti yake, Vikainua juu mikono yake.


Akasimama na kuitikisa dunia; Akatazama, mataifa yakatetemeka; Na milima ya zamani ikatawanyika; Vilima vya kale vikainama; Miendo yake ilikuwa kama siku za kale.


Na siku hiyo miguu yake itasimama juu ya mlima wa Mizeituni, unaoelekea Yerusalemu upande wa mashariki, nao mlima wa Mizeituni utapasuka katikati yake, upande wa mashariki na upande wa magharibi; litakuwako huko bonde kubwa sana; na nusu ya mlima ule utaondoka kwenda upande wa kaskazini, na nusu yake itaondoka kwenda upande wa kusini.


Na tazama, palikuwa na tetemeko kubwa la ardhi; kwa sababu malaika wa Bwana alishuka kutoka mbinguni, akaja akalivingirisha lile jiwe akalikalia.


Hata walipokwisha kumwomba Mungu, mahali pale walipokusanyika pakatikiswa, wote wakajaa Roho Mtakatifu, wakanena neno la Mungu kwa ujasiri.


Tena nijapokuwa na unabii, na kujua siri zote na maarifa yote, nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo, mimi si kitu.


Maana, moto umewashwa kwa hasira yangu, Unateketea hata chini ya kuzimu, Unakula dunia pamoja na mazao yake, Unaunguza misingi ya milima.


BWANA, ulipotoka katika Seiri, Ulipokwenda vitani kutoka mashamba ya Edomu, Nchi ilitetema, mbingu nazo zikadondosha maji, Naam, mawingu yakadondosha maji.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo