Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Zaburi 18:6 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

6 Katika shida yangu nilimwita BWANA, Na kumlalamikia Mungu wangu. Akaisikia sauti yangu hekaluni mwake, Kilio changu kikaingia masikioni mwake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

6 Katika taabu yangu nilimwita Mwenyezi-Mungu, nilimlilia Mungu wangu anisaidie. Aliisikia sauti yangu hekaluni mwake; kilio changu kilimfikia masikioni mwake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

6 Katika taabu yangu nilimwita Mwenyezi-Mungu, nilimlilia Mungu wangu anisaidie. Aliisikia sauti yangu hekaluni mwake; kilio changu kilimfikia masikioni mwake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

6 Katika taabu yangu nilimwita Mwenyezi-Mungu, nilimlilia Mungu wangu anisaidie. Aliisikia sauti yangu hekaluni mwake; kilio changu kilimfikia masikioni mwake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

6 Katika shida yangu nalimwita Mwenyezi Mungu, nilimlilia Mungu wangu anisaidie. Kutoka hekaluni mwake alisikia sauti yangu, kilio changu kikafika mbele zake, masikioni mwake.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

6 Katika shida yangu nalimwita bwana, nilimlilia Mungu wangu anisaidie. Kutoka hekaluni mwake alisikia sauti yangu, kilio changu kikafika mbele zake, masikioni mwake.

Tazama sura Nakili




Zaburi 18:6
17 Marejeleo ya Msalaba  

Katika shida yangu nilimwita BWANA, Naam, nikamlalamikia Mungu wangu; Naye akaisikia sauti yangu hekaluni mwake, Kilio changu kikaingia masikioni mwake.


Ndipo wakasimama makuhani Walawi, wakawabariki watu; ikasikiwa sauti yao, sala yao ikafika hata makao yake matakatifu, yaani, mbinguni.


BWANA yu katika hekalu lake takatifu. BWANA ambaye kiti chake kiko mbinguni, Macho yake yanaangalia; Kope zake zinawapima wanadamu.


Katika shida yangu nilimlilia BWANA Naye akaniitikia.


Macho ya BWANA huwaelekea wenye haki, Na masikio yake hukielekea kilio chao.


Bali mimi, kwa wingi wa fadhili zako, Nitaingia nyumbani mwako; Na kusujudu kwa kicho, Nikilielekea hekalu lako takatifu.


Uniite siku ya mateso; Nitakuokoa, nawe utanitukuza.


Hofu na tetemeko limenijia, Na hofu kubwa imeniingia.


Na kisha baada ya muda, yule mfalme wa Misri akafa; wana wa Israeli wakaugua kwa sababu ya ule utumwa, wakalia; kilio chao kikafika juu kwa Mungu kwa sababu ya ule utumwa.


Lakini BWANA yumo ndani ya hekalu lake takatifu; dunia yote na inyamaze kimya mbele zake.


Akasema, Aba, Baba, yote yawezekana kwako; uniondolee kikombe hiki; lakini, si kama nitakavyo mimi, bali utakavyo wewe.


Basi Petro akalindwa gerezani, nalo kanisa likamwomba Mungu kwa juhudi kwa ajili yake.


Kisha hekalu la Mungu lililoko mbinguni likafunguliwa, na sanduku la Agano lake likaonekana ndani ya hekalu lake. Kukawa na umeme, na sauti, na radi, na tetemeko la nchi, na mvua kubwa ya mawe.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo