Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Zaburi 17:7 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

7 Dhihirisha fadhili zako za ajabu Wewe uwaokoaye wanaokukimbilia; Kwa mkono wako wa kulia Uwaokoe kutoka kwa adui zao.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

7 Onesha fadhili zako za ajabu, uwaokoe kutoka kwa adui zao, wale wanaokimbilia usalama kwako.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

7 Onesha fadhili zako za ajabu, uwaokoe kutoka kwa adui zao, wale wanaokimbilia usalama kwako.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

7 Onesha fadhili zako za ajabu, uwaokoe kutoka kwa adui zao, wale wanaokimbilia usalama kwako.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

7 Uoneshe ajabu ya upendo wako mkuu, wewe unayeokoa kwa mkono wako wa kuume wale wanaokukimbilia kutokana na adui zao.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

7 Uonyeshe ajabu ya upendo wako mkuu, wewe uokoaye kwa mkono wako wa kuume wale wanaokukimbilia kutokana na adui zao.

Tazama sura Nakili




Zaburi 17:7
18 Marejeleo ya Msalaba  

Ni nani uliyemshutumu na kumtukana? Umeinua sauti yako juu ya nani, na kuinua macho yako juu? Juu ya Mtakatifu wa Israeli.


Maana nitaulinda mji huu, niuokoe, kwa ajili yangu mwenyewe, na kwa ajili ya Daudi, mtumishi wangu.


Kwa maana macho ya BWANA hukimbia kimbia duniani kote, ili ajionesha kuwa mwenye nguvu kwa ajili ya hao, waliokamilika moyo kuelekea kwake. Kwa hayo umetenda upumbavu; kwani tangu sasa utakuwa na vita.


Sasa najua kuwa BWANA amwokoa masihi wake; Atamjibu toka mbingu zake takatifu, Kwa matendo makuu ya wokovu Ya mkono wake wa kulia.


BWANA ahimidiwe; kwa maana amenitendea Fadhili za ajabu nilipozongwa kama mji wenye boma.


Nami nilisema kwa pupa yangu, Nimekatiliwa mbali na macho yako; Lakini ulisikia sauti ya kilio changu Wakati nilipokulilia.


Maana hawakuitwaa nchi kwa upanga wao, Wala hawakupata ushindi kwa mkono wao; Bali mkono wako wa kulia, naam, mkono wako, Na nuru ya uso wako, kwa kuwa ulipendezwa nao.


Ili wapenzi wako waopolewe, Utuokoe kwa mkono wako wa kulia, utuitikie.


Mbele ya baba zao alifanya mambo ya ajabu, Katika nchi ya Misri, konde la Soani.


BWANA, mkono wako wa kulia umepata fahari ya uwezo, BWANA, mkono wako wa kulia wawasetaseta adui.


usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kulia wa haki yangu.


Basi yeye, akiisha kupandishwa hadi mkono wa kulia wa Mungu, na kupokea kwa Baba ile ahadi ya Roho Mtakatifu, amekimwaga kitu hiki mnachokiona sasa na kukisikia.


Nao wauimba wimbo wa Musa, mtumwa wa Mungu, na wimbo wa Mwana-kondoo, wakisema, Ni makuu, na ya ajabu, matendo yako, Ee Bwana Mungu Mwenyezi; Ni za haki, na za kweli, njia zako, Ee Mfalme wa mataifa.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo