Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Zaburi 147:10 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

10 Hapendezwi na nguvu za farasi, Wala hairidhii miguu ya mkimbiaji.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

10 Yeye hataki nguvu za farasi, wala hapendezwi na ushujaa wa askari;

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

10 Yeye hataki nguvu za farasi, wala hapendezwi na ushujaa wa askari;

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

10 Yeye hataki nguvu za farasi, wala hapendezwi na ushujaa wa askari;

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

10 Furaha yake haipo katika nguvu za farasi, wala furaha yake kwenye miguu ya shujaa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

10 Furaha yake haipo katika nguvu za farasi, wala furaha yake kwenye miguu ya mwanadamu.

Tazama sura Nakili




Zaburi 147:10
11 Marejeleo ya Msalaba  

Sauli na Yonathani walipendwa na kupendeza Maishani wala mautini hawakutengwa; Walikuwa wepesi kuliko tai, Walikuwa hodari kuliko simba.


Je! Utamtumaini kwa sababu ana nguvu nyingi? Au, utamwachia yeye kazi yako?


Hawa wanataja magari na hawa farasi, Lakini sisi tutalitaja jina la BWANA, Mungu wetu.


Farasi huwekwa tayari kwa siku ya vita; Lakini BWANA ndiye aletaye wokovu.


Nikarudi, na kuona chini ya jua, ya kwamba si wenye mbio washindao katika michezo, wala si walio hodari washindao vitani, wala si wenye hekima wapatao chakula, wala si watu wa ufahamu wapatao mali, wala wenye ustadi wapatao upendeleo; lakini wakati na bahati huwapata wote.


Ole wao wateremkao kwenda Misri wapate msaada, na kutegemea farasi; watumainio magari kwa kuwa ni mengi, na wapanda farasi kwa kuwa ni hodari sana; lakini hawamwangalii Mtakatifu wa Israeli, wala hawamtafuti BWANA!


Lakini nitairehemu nyumba ya Yuda; nitawaokoa kwa BWANA, Mungu wao; wala sitawaokoa kwa upinde, wala kwa upanga, wala kwa silaha, wala kwa farasi, wala kwa wapanda farasi.


Lakini BWANA akamwambia Samweli, Usimtazame uso wake, wala urefu wa kimo chake; kwa maana mimi nimemkataa. BWANA haangalii kama binadamu aangaliavyo; maana wanadamu huitazama sura ya nje, bali BWANA huutazama moyo.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo