Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Zaburi 142:5 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

5 BWANA, nimekuita nikasema, Ndiwe kimbilio langu, Fungu langu katika nchi ya walio hai.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

5 Nakulilia wewe, ee Mwenyezi-Mungu! Wewe ni kimbilio langu la usalama; wewe ni riziki yangu kuu katika nchi ya walio hai.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

5 Nakulilia wewe, ee Mwenyezi-Mungu! Wewe ni kimbilio langu la usalama; wewe ni riziki yangu kuu katika nchi ya walio hai.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

5 Nakulilia wewe, ee Mwenyezi-Mungu! Wewe ni kimbilio langu la usalama; wewe ni riziki yangu kuu katika nchi ya walio hai.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

5 Ee Mwenyezi Mungu, nakulilia wewe, nasema, “Wewe ni kimbilio langu, fungu langu katika nchi ya walio hai.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

5 Ee bwana, nakulilia wewe, nasema, “Wewe ni kimbilio langu, fungu langu katika nchi ya walio hai.”

Tazama sura Nakili




Zaburi 142:5
16 Marejeleo ya Msalaba  

BWANA ndiye aliye fungu langu, Ninaahidi kuyatii maneno yake.


BWANA ndiye fungu la posho langu, Na la kikombe changu; Wewe unayaamua maisha yangu.


Naamini ya kuwa nitauona wema wa BWANA Katika nchi ya walio hai.


Wananilipa mabaya badala ya mema, Hata nafsi yangu ikaingia ukiwa.


Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, Msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso.


BWANA wa majeshi yu pamoja nasi, Mungu wa Yakobo ni kimbilio letu.


BWANA wa majeshi yu pamoja nasi, Mungu wa Yakobo ni ngome yetu.


Maana umeniponya nafsi yangu na mauti; Je! Hukuizuia miguu yangu isianguke? Ili niende mbele za Mungu Katika nuru ya walio hai.


Mwili wangu na moyo wangu hupunguka, Bali Mungu ni mwamba wa moyo wangu Na sehemu yangu milele.


Atasema, BWANA ndiye kimbilio langu na ngome yangu, Mungu wangu nitakayemtumaini.


Kisha nikarudi na kuona udhalimu wote unaotendeka chini ya jua; na tazama, machozi yao waliodhulumiwa, ambao walikuwa hawana mfariji; na upande wa wale waliowadhulumu kulikuwa na uwezo, lakini wale walikuwa hawana mfariji.


BWANA ndiye fungu langu, husema nafsi yangu, Kwa hiyo nitamtumaini yeye.


Tazama, saa inakuja, naam, imekwisha kuja, ambapo mtatawanyika kila mmoja kwao kwao, na kuniacha mimi peke yangu; lakini mimi siko peke yangu, kwa kuwa Baba yupo pamoja nami.


Lakini Bwana alisimama pamoja nami akanitia nguvu, ili kwa kazi yangu ule ujumbe utangazwe kwa utimilifu, hata wasikie Mataifa yote; nami nikaokolewa kutoka kwa kinywa cha simba.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo