Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Zaburi 140:3 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

3 Wamenoa ndimi zao na kuwa kama za nyoka, Na katika midomo yao mna sumu ya fira.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

3 Ndimi zao hatari kama za nyoka; midomoni mwao mna maneno ya sumu kama ya joka.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

3 Ndimi zao hatari kama za nyoka; midomoni mwao mna maneno ya sumu kama ya joka.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

3 Ndimi zao hatari kama za nyoka; midomoni mwao mna maneno ya sumu kama ya joka.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

3 Wao hufanya ndimi zao kali kama za nyoka, sumu ya nyoka iko midomoni mwao.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

3 Wao hufanya ndimi zao kali kama za nyoka, sumu ya nyoka iko midomoni mwao.

Tazama sura Nakili




Zaburi 140:3
18 Marejeleo ya Msalaba  

BWANA Mungu akamwambia mwanamke, Nini hili ulilolifanya? Mwanamke akasema, Nyoka alinidanganya, nikala.


Nafsi yangu i kati ya simba, Nitastarehe kati yao waliowaka moto. Wanadamu meno yao ni mikuki na mishale, Na ndimi zao ni upanga mkali.


Wana sumu mfano wa sumu ya nyoka; Wao ni kama fira kiziwi azibaye sikio lake.


Tazama, kwa vinywa vyao huteuka, Midomoni mwao mna panga, Kwa maana ni nani asikiaye?


Kuna anenaye bila kufikiri, kama kuchoma kwa upanga; Bali ulimi wa mwenye haki ni afya.


Mwisho wake huuma kama nyoka; Huchoma kama fira.


Mna upotovu moyoni mwake, hutunga uovu daima, Hupanda mbegu za magomvi.


katika kukosa na kumkana BWANA, na katika kugeuka tusimfuate Mungu wetu, tukinena udhalimu na uasi, na kukusudia maneno ya uongo na kuyatoa moyoni.


Huupinda ulimi wao, kana kwamba ni upinde, ili kusema uongo; nao wamepata nguvu katika nchi, lakini si katika uaminifu; maana huendelea toka ubaya hata ubaya, wala hawanijui mimi, asema BWANA.


Nao watadanganya kila mtu jirani yake, wala hawatasema kweli; wameuzoesha ulimi wao kusema uongo; hujidhoofisha ili kutenda uovu.


Midomo yao walioinuka juu yangu Na maazimio yao juu yangu mchana kutwa.


Enyi wazawa wa nyoka, mwawezaje kunena mema, mkiwa wabaya? Maana, kinywa cha mtu huyanena yaujazayo moyo wake.


Lakini nahofu; kama yule nyoka alivyomdanganya Hawa kwa hila yake, asije akawaharibu fikira zenu, mkauacha unyofu na usafi kwa Kristo.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo