Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Zaburi 139:24 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

24 Uone kama iko njia iletayo majuto ndani yangu, Ukaniongoze katika njia ya milele.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

24 Uangalie kama mwenendo wangu ni mbaya, uniongoze katika njia ya milele.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

24 Uangalie kama mwenendo wangu ni mbaya, uniongoze katika njia ya milele.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

24 Uangalie kama mwenendo wangu ni mbaya, uniongoze katika njia ya milele.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

24 Uone kama kuna njia iletayo machukizo ndani yangu, uniongoze katika njia ya milele.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

24 Uone kama kuna njia iletayo machukizo ndani yangu, uniongoze katika njia ya milele.

Tazama sura Nakili




Zaburi 139:24
17 Marejeleo ya Msalaba  

Heri walio kamili njia zao, Waendao katika sheria ya BWANA.


Nitakwenda mbio katika njia ya maagizo yako, Utakaponipanulia ufahamu wangu.


Unifundishe kuyatenda mapenzi yako, Kwa maana ndiwe Mungu wangu; Roho yako mwema aniongoze katika njia iliyo sawa,


Uniwezeshe kusikia fadhili zako asubuhi, Kwa maana nimekutumaini Wewe. Unifundishe njia nitakayoiendea, Kwa maana ninakuinulia nafsi yangu.


Utanijulisha njia ya uzima; Mbele za uso wako kuna furaha tele; Na katika mkono wako wa kulia Mna mema ya milele.


Umenijaribu moyo wangu, umenijia usiku, Umenichunguza usione neno; Nimenuia kinywa changu kisikose,


Ee BWANA, unifundishe njia yako, Na kuniongoza katika njia iliyonyoka; Kwa sababu yao wanaoniotea;


BWANA, uniongoze kwa haki yako, Kwa sababu yao wanaoniotea. Uinyoshe njia yako mbele ya uso wangu,


Njia ya mtu mbaya ni chukizo kwa BWANA; Bali humpenda mtu afuatiaye wema.


Mwenye kujitumainia moyo wake ni mjinga; Bali yeye aendaye kwa busara ataokolewa.


Bali mlango ni mwembamba, na njia imebana iendayo uzimani, nao waionao ni wachache.


Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.


Basi kama mlivyompokea Kristo Yesu, Bwana, ishini vivyo hivyo katika yeye;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo