Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Zaburi 139:19 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

19 Ee Mungu, laiti ungewaua waovu! Na laiti watu wa damu wangetoka kwangu;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

19 Laiti, ee Mungu, ungewaua watu waovu! Laiti watu wauaji wangeondoka kwangu!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

19 Laiti, ee Mungu, ungewaua watu waovu! Laiti watu wauaji wangeondoka kwangu!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

19 Laiti, ee Mungu, ungewaua watu waovu! Laiti watu wauaji wangeondoka kwangu!

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

19 Laiti ungewachinja waovu, Ee Mungu! Ondokeni kwangu, ninyi wamwaga damu!

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

19 Laiti ungewachinja waovu, Ee Mungu! Ondokeni kwangu, ninyi wamwaga damu!

Tazama sura Nakili




Zaburi 139:19
12 Marejeleo ya Msalaba  

Enyi watenda mabaya, ondokeni kwangu, Niyashike maagizo ya Mungu wangu.


Utawaharibu wasemao uongo; BWANA humchukia mwuaji na mwenye hila


Nawe, Ee Mungu, utawateremsha, Wafikie shimo la uharibifu; Watu wa damu na hila hawataishi nusu ya siku zao, Bali mimi nitakutumaini Wewe.


Ondokeni kwangu, ninyi nyote mtendao uovu; Kwa kuwa BWANA ameisikia sauti ya kilio changu.


Lakini Mungu atawapiga kwa mshale wake, Na kuwajeruhi ghafla.


Wadhalimu wataenda kuzimu, Naam, mataifa yote wanaomsahau Mungu.


Kwa maana mhitaji hatasahauliwa daima; Matumaini ya wanyonge hayatapotea milele.


Naye atawarudishia uovu wao, Atawaangamiza katika ubaya wao, Naam, BWANA, Mungu wetu, atawaangamiza.


bali kwa haki atawahukumu maskini, naye atawaonya wanyenyekevu wa dunia kwa adili; naye ataipiga dunia kwa fimbo ya kinywa chake, na kwa pumzi ya midomo yake atawaua wabaya.


Kisha atawaambia na wale walioko katika mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake;


Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu.


Kwa hiyo, Tokeni kati yao, Mkatengwe nao, asema Bwana, Msiguse kitu kilicho kichafu, Nami nitawakaribisha.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo