Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Zaburi 137:7 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

7 Ee BWANA, uwakumbuke wana wa Edomu, Siku ile Yerusalemu ilipotekwa. Kwa namna walivyosema, Bomoeni! Bomoeni hata misingini!

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

7 Ee Mwenyezi-Mungu, usisahau waliyotenda Waedomu, siku ile Yerusalemu ilipotekwa; kumbuka waliyosema: “Bomoeni mji wa Yerusalemu! Ngoeni hata na misingi yake!”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

7 Ee Mwenyezi-Mungu, usisahau waliyotenda Waedomu, siku ile Yerusalemu ilipotekwa; kumbuka waliyosema: “Bomoeni mji wa Yerusalemu! Ngoeni hata na misingi yake!”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

7 Ee Mwenyezi-Mungu, usisahau waliyotenda Waedomu, siku ile Yerusalemu ilipotekwa; kumbuka waliyosema: “Bomoeni mji wa Yerusalemu! Ng'oeni hata na misingi yake!”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

7 Kumbuka, Ee Mwenyezi Mungu, walichokifanya Waedomu, siku ile Yerusalemu ilipoanguka. Walisema, “Bomoa, bomoa hata misingi yake!”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

7 Kumbuka, Ee bwana, walichokifanya Waedomu, siku ile Yerusalemu ilipoanguka. Walisema, “Bomoa, Bomoa mpaka kwenye misingi yake!”

Tazama sura Nakili




Zaburi 137:7
17 Marejeleo ya Msalaba  

Uwakumbuke, Ee Mungu wangu, Tobia na Sanbalati kulingana na hayo matendo yao, na yule nabii mwanamke Noadia.


Ee BWANA, uyakumbuke hayo, adui amelaumu, Na watu wapumbavu wamelidharau jina lako.


BWANA akamwambia Musa, Andika habari hii katika kitabu iwe ukumbusho, kisha ihubiri masikioni mwa Yoshua; ya kuwa nitaufuta ukumbusho wa Amaleki kabisa, usiwe tena chini ya mbingu.


Kama vile ulivyofurahi juu ya urithi wa nyumba ya Israeli, kwa sababu ilikuwa ukiwa, ndivyo nitakavyokutenda wewe; utakuwa ukiwa, Ee mlima Seiri, na Edomu yote, naam, yote pia; nao watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA.


Mwanadamu, kaza uso wako juu ya mlima Seiri, ukatabiri juu yake,


Wala hawafikiri mioyoni mwao ya kwamba naukumbuka uovu wao wote; sasa matendo yao wenyewe yamewazunguka pande zote; yako mbele za uso wangu.


Haya ndiyo asemayo BWANA; Kwa makosa matatu ya Edomu, naam, kwa manne, sitaizuia adhabu yake isimpate; kwa sababu alimfuatia ndugu yake kwa upanga, akatupilia mbali huruma zake zote; hasira yake ikararuararua daima, akaishika ghadhabu yake milele;


Ukatokea kwa ajili ya wokovu wa watu wako, Kwa ajili ya wokovu wa masihi wako; Ukakiponda kichwa cha nyumba ya waovu, Ukiuweka wazi msingi hata mwambani.


BWANA wa majeshi asema hivi, Nimeyatia moyoni mwangu yale ambayo Waamaleki waliwatenda Waisraeli, jinsi walivyowapinga njiani, hapo walipopanda kutoka Misri.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo