Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Zaburi 134:1 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

1 Njoni, enyi watumishi wote wa BWANA, Mhimidini BWANA Ninyi mnaohudumu usiku Katika nyumba ya BWANA.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 Njoni kumsifu Mwenyezi-Mungu enyi watumishi wake wote, enyi nyote mnaotumikia usiku nyumbani mwake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 Njoni kumsifu Mwenyezi-Mungu enyi watumishi wake wote, enyi nyote mnaotumikia usiku nyumbani mwake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Njoni kumsifu Mwenyezi-Mungu enyi watumishi wake wote, enyi nyote mnaotumikia usiku nyumbani mwake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Msifuni Mwenyezi Mungu, ninyi nyote watumishi wa Mwenyezi Mungu, ninyi mnaotumika usiku ndani ya nyumba ya Mwenyezi Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Msifuni bwana, ninyi nyote watumishi wa bwana, ninyi mnaotumika usiku ndani ya nyumba ya bwana.

Tazama sura Nakili




Zaburi 134:1
32 Marejeleo ya Msalaba  

Basi watu hao na wana wao walikuwa na kazi ya ulinzi wa malango ya nyumba ya BWANA, yaani, nyumba ya maskani, kwa zamu.


Nao walilala kandokando nyumbani mwa Mungu, kwa kuwa ulinzi wake ulikuwa juu yao, nayo ilikuwa kazi yao kuyafungua malango kila siku asubuhi.


Tena hawa ndio waimbaji, wakuu wa koo za baba zao katika Walawi, ambao walikaa vyumbani, kisha walikuwa hawana kazi nyingine; kwa kuwa walifanya kazi yao mchana na usiku.


Basi wanangu, msiyapuuze haya, kwa kuwa BWANA amewachagua ninyi msimame mbele yake, kumhudumia, nanyi mpate kuwa watumishi wake, mkafukize uvumba.


Mkasimame katika patakatifu, kama ndugu zenu wana wa watu walivyogawanyika kufuata nyumba za mababa, kadiri ya mgawanyiko wa kila nyumba ya baba, ya Walawi.


Tena Bakbukia na Uno, washiriki wenzao walisimama mkabala wao.


Mhimidini BWANA, enyi majeshi yake yote, Ninyi watumishi wake mfanyao mapenzi yake.


Haleluya. Enyi watumishi wa BWANA, sifuni, Lisifuni jina la BWANA.


Katika shida yangu nilimlilia BWANA Naye akaniitikia.


Nayainua macho yangu niitazame milima, Msaada wangu utatoka wapi?


Nilifurahi waliponiambia, Twende nyumbani kwa BWANA.


Nimekuinulia macho yangu, Wewe uketiye mbinguni.


Kama si BWANA aliyekuwa pamoja nasi, Israeli na aseme sasa,


Wamtumainio BWANA ni kama mlima Sayuni, Ambao hautikisiki, wakaa milele.


BWANA alipowarejesha mateka wa Sayuni, Tulikuwa kama waotao ndoto.


BWANA asipoijenga nyumba Waijengao wanafanya kazi bure. BWANA asipoulinda mji Yeye aulindaye anakesha bure.


Heri kila mtu amchaye BWANA, Aendaye katika njia yake.


Mara nyingi wamenitesa tangu ujana wangu, Israeli na aseme sasa,


Ee BWANA, toka vilindini nimekulilia.


Nafsi yangu inamngoja Bwana, Kuliko walinzi waingojavyo asubuhi, Naam, walinzi waingojao asubuhi.


BWANA, moyo wangu hauna kiburi, Wala macho yangu hayainuki. Wala sijishughulishi na mambo makuu, Wala mambo yanayozidi nguvu zangu.


BWANA, umkumbukie Daudi Taabu zake zote alizotaabika.


Tazama, jinsi ilivyo vyema, na kupendeza, Ndugu kuishi pamoja, kwa umoja.


Heri ambaye nguvu zake zatoka kwako, Na njia ziendazo Sayuni zimo moyoni mwake.


Nanyi mtakaa mlangoni pa hema ya kukutania muda wa siku saba mchana na usiku, na kuulinda ulinzi wa BWANA ili kwamba msife; kwani ndivyo nilivyoagizwa.


Naye ni mjane wa miaka themanini na minne; haondoki katika hekalu, ila huabudu usiku na mchana kwa kufunga na kuomba.


Na wakati huo BWANA alilitenga kabila la Lawi ili walichukue lile sanduku la Agano la BWANA, wasimame mbele ya BWANA kwa kumtumikia, na kuwabarikia watu kwa jina lake, hata hivi leo.


Sauti ikatoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Msifuni Mungu wetu, enyi watumwa wake wote, ninyi mnaomcha, wadogo kwa wakubwa.


Kwa hiyo wako mbele ya kiti cha enzi cha Mungu, nao wanamtumikia mchana na usiku katika hekalu lake, na yeye aketiye katika kiti cha enzi atatanda hema yake juu yao.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo