Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Zaburi 130:5 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

5 Nimemngoja BWANA, roho yangu imengoja, Na neno lake nimelitumainia.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

5 Namtumainia Mwenyezi-Mungu kwa moyo wangu wote; nina imani sana na neno lake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

5 Namtumainia Mwenyezi-Mungu kwa moyo wangu wote; nina imani sana na neno lake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

5 Namtumainia Mwenyezi-Mungu kwa moyo wangu wote; nina imani sana na neno lake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

5 Namngojea Mwenyezi Mungu, nafsi yangu inangojea, katika neno lake naweka tumaini langu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

5 Namngojea bwana, nafsi yangu inangojea, katika neno lake naweka tumaini langu.

Tazama sura Nakili




Zaburi 130:5
17 Marejeleo ya Msalaba  

Wokovu wako nimeungoja, Ee BWANA.


Ndiwe sitara yangu na ngao yangu, Neno lako nimelingojea.


Nami nitamjibu neno anilaumuye, Kwa maana nilitumainia neno lako.


Likumbuke neno ulilomwambia mtumishi wako, Ambalo kwalo umenipa tumaini.


Wakuchao na wanione na kufurahi, Kwa sababu nimelitumainia neno lako.


Nafsi yangu imefifia kwa kuutamani wokovu wako, Nimelitumainia neno lako.


Umtumainie BWANA, uwe imara, Upige moyo konde, naam, umngoje BWANA.


Nafsi zetu zinamngoja BWANA; Yeye ndiye msaada wetu na ngao yetu.


Nilimngoja BWANA kwa subira, Akaniinamia na kusikia kilio changu.


Nafsi yangu yamngoja Mungu peke yake kwa utulivu, Wokovu wangu hutoka kwake.


Nafsi yangu, umngoje Mungu peke yake kwa utulivu. Maana tumaini langu hutoka kwake.


Naam, katika njia ya hukumu zako Sisi tumekungoja, Ee BWANA; Shauku ya nafsi zetu inaelekea Jina lako na ukumbusho wako.


Kwa ajili ya hayo BWANA atangoja, ili awaonee huruma, na kwa ajili ya hayo atatukuzwa, ili awarehemu; kwa maana BWANA ni Mungu wa hukumu; heri wote wamngojao.


Nami nitamngojea BWANA, awafichaye uso wake nyumba ya Yakobo, nami nitamtazamia.


Na tazama, pale Yerusalemu palikuwa na mtu, jina lake Simeoni, naye ni mtu mwenye haki, mcha Mungu, akiitarajia faraja ya Israeli; na Roho Mtakatifu alikuwa juu yake.


Huyu alitokea saa ile ile akamshukuru Mungu, na wote waliokuwa wakiutarajia ukombozi katika Yerusalemu akawatolea habari zake.


ili kwa vitu viwili visivyoweza kubadilika, ambavyo katika hivyo Mungu hawezi kusema uongo, tupate faraja iliyo imara, sisi tuliokimbilia kuyashika matumaini yale yawekwayo mbele yetu;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo