Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Zaburi 130:2 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

2 Bwana, uisikie sauti yangu. Masikio yako na yaisikilize Sauti ya dua zangu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

2 Ee Bwana, sikia sauti yangu, uitegee sikio sauti ya ombi langu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

2 Ee Bwana, sikia sauti yangu, uitegee sikio sauti ya ombi langu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

2 Ee Bwana, sikia sauti yangu, uitegee sikio sauti ya ombi langu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

2 Ee Bwana, sikia sauti yangu. Masikio yako na yawe masikivu kwa kilio changu unihurumie.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

2 Ee bwana, sikia sauti yangu. Masikio yako na yawe masikivu kwa kilio changu unihurumie.

Tazama sura Nakili




Zaburi 130:2
13 Marejeleo ya Msalaba  

Na sasa, Ee Mungu wangu, macho yako yafumbuke, nakusihi, masikio yako yakasikilize maombi yaombwayo mahali hapa.


Ee Bwana, nakusihi, litege sikio lako, uyasikilize maombi ya mtumishi wako, na maombi ya watumishi wako, wanaofurahi kulicha jina lako; nakuomba sana; unifanikishe mimi, mtumishi wako, leo, ukanijalie rehema mbele ya mtu huyu. (Maana, nilikuwa mnyweshaji wa mfalme).


tega sikio lako, macho yako yakafumbuke, upate kuyasikiliza maombi ya mtumishi wako, ninayoomba mbele zako wakati huu, mchana na usiku, kwa ajili ya wana wa Israeli, watumishi wako; hapo ninapoziungama dhambi za wana wa Israeli, tulizozifanya juu yako; naam, mimi na nyumba ya baba yangu tumefanya dhambi.


Nimemwambia BWANA, Ndiwe Mungu wangu; Ee BWANA, uisikie sauti ya dua zangu.


Ee BWANA, usikie haki, ukisikilize kilio changu, Utege sikio lako kwa maombi yangu, Yasiyotoka katika midomo ya hila.


Uisikie sauti ya dua yangu nikuombapo, Nikipainulia patakatifu pako mikono yangu.


BWANA, asubuhi utaisikia sauti yangu, Asubuhi nitakupangia dua yangu na kutazamia.


Mungu, uisikie sauti yangu katika malalamiko yangu; Unilinde uhai wangu kutoka kwa hofu ya adui.


Tega sikio lako, BWANA, usikie; funua macho yako, BWANA, uone; uyasikie maneno ya Senakeribu, aliyopeleka ili kumtukana Mungu aliye hai.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo