Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Zaburi 121:8 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

8 BWANA atakulinda utokapo na uingiapo, Tangu sasa na hata milele.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

8 Mwenyezi-Mungu atakulinda katika shughuli zako zote tangu sasa na hata milele.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

8 Mwenyezi-Mungu atakulinda katika shughuli zako zote tangu sasa na hata milele.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

8 Mwenyezi-Mungu atakulinda katika shughuli zako zote tangu sasa na hata milele.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

8 Mwenyezi Mungu atakulinda unapoingia na unapotoka, tangu sasa na hata milele.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

8 bwana atakulinda unapoingia na unapotoka, tangu sasa na hata milele.

Tazama sura Nakili




Zaburi 121:8
12 Marejeleo ya Msalaba  

Zamani za kale, hapo Sauli alipokuwa mfalme juu yetu, wewe ndiwe uliyewaongoza Israeli wakitoka nje kwenda, na kurudi vitani. Naye BWANA akakuambia, Wewe utawalisha watu wangu Israeli, nawe utakuwa mkuu juu ya Israeli.


Ndipo nikaamuru kufunga, hapo penye mto Ahava, ili tupate kujinyenyekeza mbele za Mungu, na kutafuta kwake njia iliyonyoka, kwa ajili yetu sisi wenyewe, na kwa ajili ya watoto wetu, na kwa mali yetu yote.


Ndipo tukasafiri toka mtoni Ahava siku ya kumi na mbili ya mwezi wa kwanza, ili kwenda Yerusalemu; na mkono wa Mungu ulikuwa pamoja nasi, akatuokoa na mkono wa adui, na mtu mwenye kutuvizia njiani.


Jina la BWANA lihimidiwe Tangu leo na hata milele.


Bali sisi tutamhimidi BWANA, Tangu leo na hata milele.


Kama milima inavyouzunguka Yerusalemu, Ndivyo BWANA anavyowazunguka watu wake, Tangu sasa na hata milele.


Ee Israeli, umtarajie BWANA, Tangu leo na hata milele.


Apate kuyalinda mapito ya hukumu, Na kuhifadhi njia ya watakatifu wake.


Katika njia zako zote mkiri yeye, Naye atayanyosha mapito yako.


Utalaaniwa uingiapo, utalaaniwa na utokapo,


Utabarikiwa uingiapo, utabarikiwa na utokapo.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo