Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Zaburi 119:174 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

174 Ee BWANA, nimeutamani wokovu wako, Na sheria yako ndiyo furaha yangu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

174 Natazamia sana uniokoe, ee Mwenyezi-Mungu; sheria yako ndiyo furaha yangu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

174 Natazamia sana uniokoe, ee Mwenyezi-Mungu; sheria yako ndiyo furaha yangu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

174 Natazamia sana uniokoe, ee Mwenyezi-Mungu; sheria yako ndiyo furaha yangu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

174 Ee Mwenyezi Mungu, ninatamani wokovu wako, na sheria yako ni furaha yangu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

174 Ee bwana, ninatamani wokovu wako, na sheria yako ni furaha yangu.

Tazama sura Nakili




Zaburi 119:174
17 Marejeleo ya Msalaba  

Wokovu wako nimeungoja, Ee BWANA.


Je! Sivyo ilivyo nyumba yangu mbele za BWANA? Kwa kuwa amefanya nami agano la milele; Ina taratibu katika yote, ni thabiti, Maana ni wokovu wangu wote, na shauku langu lote.


Bali sheria ya BWANA ndiyo impendezayo, Na sheria yake huitafakari mchana na usiku.


Shuhuda zako nimezifanya urithi wa milele, Maana ndizo changamko la moyo wangu.


Nitajifurahisha sana kwa amri zako, Sitalisahau neno lako.


Naifurahia ahadi yako, Kama apataye mateka mengi.


Shuhuda zako nazo ndizo furaha yangu, Na washauri wangu.


Ee BWANA, fadhili zako zinifikie na mimi, Naam, wokovu wako kulingana na ahadi yako.


Nami nitajifurahisha sana kwa maagizo yako, Ambayo nimeyapenda.


Rehema zako zinijie nipate kuishi, Maana sheria yako ni furaha yangu.


Nafsi yangu imefifia kwa kuutamani wokovu wako, Nimelitumainia neno lako.


Kilichotarajiwa kikikawia kuja, moyo huugua. Bali haja ya mtu ikipatikana, ni mti wa uzima.


Nawasihi, enyi binti za Yerusalemu, Ninyi mkimwona mpendwa wangu, Ni nini mtakayomwambia? Ya kwamba nazimia kwa mapenzi.


Ninasongwa katikati ya mambo mawili; ninatamani kwenda zangu nikae na Kristo maana ni vizuri zaidi sana;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo