Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Zaburi 119:132 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

132 Unigeukie na kunirehemu, Kama ilivyo desturi yako kwa walipendalo jina lako.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

132 Unigeukie na kunionea huruma, kama uwatendeavyo wanaokupenda.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

132 Unigeukie na kunionea huruma, kama uwatendeavyo wanaokupenda.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

132 Unigeukie na kunionea huruma, kama uwatendeavyo wanaokupenda.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

132 Nigeukie na unihurumie, kama uwafanyiavyo siku zote wale wanaolipenda jina lako.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

132 Nigeukie na unihurumie, kama uwafanyiavyo siku zote wale wanaolipenda jina lako.

Tazama sura Nakili




Zaburi 119:132
10 Marejeleo ya Msalaba  

Labda BWANA atayaangalia mabaya yaliyonipata, naye BWANA atanilipa mema kwa sababu ya kunilaani kwake leo.


Ee BWANA, unikumbuke mimi, Kwa kibali ulicho nacho kwa watu wako. Unijie kwa wokovu wako,


Kama zilivyo rehema zako umtendee mtumishi wako, Na amri zako unifundishe.


Uniangalie na kunifadhili, Maana mimi ni mkiwa na mteswa.


Utazame mateso yangu na taabu yangu; Unisamehe dhambi zangu zote.


Kwa maana Wewe utambariki mwenye haki; BWANA, utamzungushia radhi kama ngao.


Watu wakaamini, na waliposikia ya kuwa BWANA amewajia wana wa Israeli, na ya kuwa ameyaona mateso yao, wakainamisha vichwa vyao wakasujudu.


Akaweka nadhiri, akasema, Ee BWANA wa majeshi, ikiwa wewe utayaangalia mateso la mjakazi wako, na kunikumbuka, wala usinisahau mimi mjakazi wako, na kunipa mimi mjakazi wako mtoto wa kiume, ndipo mimi nitakapompa BWANA huyo mtoto siku zote za maisha yake, wala wembe hautamfikia kichwani kamwe.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo