Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Zaburi 119:108 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

108 Ee BWANA, uziridhie sadaka za kinywa changu, Na kunifundisha hukumu zako.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

108 Ee Mwenyezi-Mungu, upokee sala yangu ya shukrani; na kunifundisha maagizo yako.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

108 Ee Mwenyezi-Mungu, upokee sala yangu ya shukrani; na kunifundisha maagizo yako.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

108 Ee Mwenyezi-Mungu, upokee sala yangu ya shukrani; na kunifundisha maagizo yako.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

108 Ee Mwenyezi Mungu, pokea sifa za hiari za kinywa changu, nifundishe sheria zako.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

108 Ee bwana, pokea sifa za hiari za kinywa changu, nifundishe sheria zako.

Tazama sura Nakili




Zaburi 119:108
9 Marejeleo ya Msalaba  

Na Kore, mwana wa Imna, Mlawi, bawabu wa mlango wa mashariki, alizisimamia sadaka za hiari za Mungu; ili kugawa matoleo ya BWANA, na vitu vilivyokuwa vitakatifu sana.


Ee BWANA, umehimidiwa, Unifundishe amri zako.


Kufafanuliwa kwa maneno yako kunatia nuru, Na kumfahamisha mjinga.


Ee BWANA, kilio changu na kikufikie, Unifahamishe sawasawa na neno lako.


Nilizisimulia njia zangu ukanijibu, Unifundishe amri zako.


Na sasa kichwa changu kitainuka Juu ya adui zangu wanaonizunguka. Nami nitatoa dhabihu za shangwe hemani mwake; Nitaimba, naam, nitamhimidi BWANA.


Chukueni maneno pamoja nanyi, mkamrudie BWANA; mkamwambie, Ondoa maovu yote, uyatakabali yaliyo mema; na hivyo ndivyo mtakavyotoa sadaka za midomo yetu kana kwamba ni ng'ombe.


Sadaka hizo mtamsogezea BWANA katika sikukuu zenu zilizoamriwa, zaidi ya nadhiri zenu, na sadaka zenu za hiari, kuwa sadaka zenu za kuteketezwa, na sadaka zenu za unga, na sadaka zenu za vinywaji, na sadaka zenu za amani.


Basi, kwa njia yake yeye, na tumpe Mungu dhabihu ya sifa daima, yaani, tunda la midomo iliungamalo jina lake.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo