Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Zaburi 118:15 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

15 Sauti ya furaha na wokovu Imo hemani mwao wenye haki; Mkono wa kulia wa BWANA hutenda makuu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

15 Sauti za furaha ya ushindi zasikika hemani mwao waadilifu: “Mkono wa Mwenyezi-Mungu umetenda mambo makuu!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

15 Sauti za furaha ya ushindi zasikika hemani mwao waadilifu: “Mkono wa Mwenyezi-Mungu umetenda mambo makuu!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

15 Sauti za furaha ya ushindi zasikika hemani mwao waadilifu: “Mkono wa Mwenyezi-Mungu umetenda mambo makuu!

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

15 Sauti za shangwe na ushindi zinavuma kwenye hema za wenye haki: “Mkono wa kuume wa Mwenyezi Mungu umetenda mambo makuu!

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

15 Sauti za shangwe na ushindi zinavuma hemani mwa wenye haki: “Mkono wa kuume wa bwana umetenda mambo makuu!

Tazama sura Nakili




Zaburi 118:15
21 Marejeleo ya Msalaba  

Matendo ya BWANA ni makuu, Yafikiriwa sana na wapendezwao nayo.


Shuhuda zako nimezifanya urithi wa milele, Maana ndizo changamko la moyo wangu.


Amri zako zimekuwa nyimbo zangu, Katika nyumba yangu ya ugenini.


Mfurahieni BWANA; Shangilieni, enyi wenye haki Pigeni vigelegele vya furaha; Ninyi nyote mlio wanyofu wa moyo.


Maana hawakuitwaa nchi kwa upanga wao, Wala hawakupata ushindi kwa mkono wao; Bali mkono wako wa kulia, naam, mkono wako, Na nuru ya uso wako, kwa kuwa ulipendezwa nao.


Katika fahari yako usitawi uendelee Kwa ajili ya kweli, upole na haki Na mkono wako wa kulia Utakutendea mambo ya ajabu.


Kwa maana Wewe utambariki mwenye haki; BWANA, utamzungushia radhi kama ngao.


Kwa msaada wa Mungu tutatenda makuu, Maana Yeye atawakanyaga watesi wetu.


Bali wenye haki hufurahi, Na kuushangilia uso wa Mungu, Naam, hupiga kelele kwa furaha.


Mkono wako ni mkono wenye uweza, Mkono wako una nguvu, Mkono wako wa kulia umetukuka.


Mwimbieni BWANA wimbo mpya, Kwa maana ametenda mambo ya ajabu. Mkono wa kulia, Na mkono wake mtakatifu umemtendea wokovu.


BWANA, mkono wako wa kulia umepata fahari ya uwezo, BWANA, mkono wako wa kulia wawasetaseta adui.


Kwa hiyo Bwana MUNGU asema hivi, Tazama, watumishi wangu watakula, bali ninyi mtaona njaa; tazama, watumishi wangu watakunywa, bali ninyi mtaona kiu; tazama, watumishi wangu watafurahi, bali ninyi mtatahayarika;


Amefanya nguvu kwa mkono wake; Amewatawanya walio na kiburi katika mawazo ya mioyo yao;


Akawaleta juu nyumbani kwake, akawaandalia chakula, akafurahi sana, yeye na nyumba yake yote, maana amekwisha kumwamini Mungu.


Nanyi mtafurahi mbele za BWANA, Mungu wenu, ninyi, na wana wenu, na binti zenu, na watumishi wenu wa kiume na wa kike, na Mlawi aliyemo malangoni mwenu; kwa kuwa hana sehemu wala urithi kwenu.


Furahini juu yake, enyi mbingu, na enyi watakatifu, mitume na manabii; kwa maana Mungu ametoa hukumu kwa ajili yenu juu yake.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo