Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Zaburi 116:6 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

6 BWANA huwalinda wasio na hila; Nilidhilika, akaniokoa.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

6 Mwenyezi-Mungu huwalinda wanyofu; nilipokuwa nimekandamizwa aliniokoa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

6 Mwenyezi-Mungu huwalinda wanyofu; nilipokuwa nimekandamizwa aliniokoa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

6 Mwenyezi-Mungu huwalinda wanyofu; nilipokuwa nimekandamizwa aliniokoa.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

6 Mwenyezi Mungu huwalinda wanyenyekevu, nilipokuwa katika shida kubwa, aliniokoa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

6 bwana huwalinda wanyenyekevu, nilipokuwa katika shida kubwa, aliniokoa.

Tazama sura Nakili




Zaburi 116:6
11 Marejeleo ya Msalaba  

Mara nyingi aliwaponya, Bali walikuwa wakimwasi kwa mashauri yao, Wakawa dhalili kwa uovu wao.


Ukisikilize kilio changu, Kwa maana nimedhilika sana. Uniponye kutoka kwa wanaonifuatia, Kwa maana wao ni hodari kuliko mimi.


Sheria ya BWANA ni kamilifu, Huiburudisha nafsi. Ushuhuda wa BWANA ni amini, Humtia hekima mtu asiye nayo.


Ukamilifu na unyofu zinihifadhi, Maana nakungoja Wewe.


Usikumbuke juu yetu maovu ya baba zetu, Rehema zako zije kutulaki haraka, Kwa maana tumeteseka sana.


Na hapo patakuwa na njia kuu, na njia, nayo itaitwa, Njia ya utakatifu; wasio safi hawatapita juu yake; bali itakuwa kwa ajili ya watu hao; wasafirio, wajapokuwa wajinga, hawatapotea katika njia hiyo.


Wakati ule Yesu akajibu, akasema, Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa mambo haya uliwaficha wenye hekima na akili, ukawafunulia watoto wachanga.


Maana utii wenu umewafikia watu wote; basi nafurahi kwa ajili yenu, lakini nataka ninyi kuwa wenye hekima katika mambo mema, na wasio na hatia katika mambo mabaya.


Kwa maana kujisifu kwetu ni huku, ushuhuda wa dhamiri yetu, ya kwamba kwa utakatifu na weupe wa moyo utokao kwa Mungu; si kwa hekima ya mwili, bali kwa neema ya Mungu; tulienenda katika dunia, na hasa kwenu ninyi.


Lakini nahofu; kama yule nyoka alivyomdanganya Hawa kwa hila yake, asije akawaharibu fikira zenu, mkauacha unyofu na usafi kwa Kristo.


Ninyi watumwa, watiini hao ambao kwa mwili ni bwana zenu, katika mambo yote, si kwa utumwa wa macho, kama wajipendekezao kwa wanadamu, bali kwa unyofu wa moyo, mkimcha Bwana.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo