Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Zaburi 112:1 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

1 Haleluya. Heri mtu yule amchaye BWANA, Apendezwaye sana na maagizo yake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 Msifuni Mwenyezi-Mungu! Heri mtu anayemcha Mwenyezi-Mungu, anayefurahia sana kutii amri zake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 Msifuni Mwenyezi-Mungu! Heri mtu anayemcha Mwenyezi-Mungu, anayefurahia sana kutii amri zake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Msifuni Mwenyezi-Mungu! Heri mtu anayemcha Mwenyezi-Mungu, anayefurahia sana kutii amri zake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Msifuni Mwenyezi Mungu. Heri mtu yule amchaye Mwenyezi Mungu, mtu yule apendezwaye sana na amri zake.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Msifuni bwana. Heri mtu yule amchaye bwana, mtu yule apendezwaye sana na amri zake.

Tazama sura Nakili




Zaburi 112:1
25 Marejeleo ya Msalaba  

Ahabu akamwita Obadia, aliyekuwa juu ya nyumba yake; (na huyu Obadia alikuwa mwenye kumcha BWANA sana;


Haleluya. Nitamshukuru BWANA kwa moyo wangu wote, Barazani pa wanyofu wa moyo na katika mkutano.


Kumcha BWANA ndio mwanzo wa hekima, Wote wafanyao hayo wana ufahamu mzuri, Sifa zake zadumu milele.


Nimeifurahia njia ya shuhuda zako Kana kwamba ni mali mengi.


Taabu na dhiki zimenipata, Maagizo yako ni furaha yangu.


Nitajifurahisha sana kwa amri zako, Sitalisahau neno lako.


Uniendeshe katika mapito ya amri zako, Kwa maana nimependezwa nayo.


Sheria yako naipenda mno ajabu, Ndiyo kutafakari kwangu mchana kutwa.


Heri kila mtu amchaye BWANA, Aendaye katika njia yake.


Hutimiza matakwa ya wote wamchao, Na pia husikia kilio chao, na huwaokoa.


Haleluya. Msifuni Bwana; Maana ni vema kumwimbia Mungu wetu sifa, Maana ni mwenye fadhili, na anastahili kuimbiwa sifa.


Haleluya. Msifuni Mungu katika patakatifu pake; Msifuni katika anga la uweza wake.


Kuyafanya mapenzi yako, Ee Mungu wangu, ndiyo furaha yangu; Naam, sheria yako imo moyoni mwangu.


Ilikuwa kwa sababu wale wakunga walikuwa wakimcha Mungu, akawasimamishia nyumba.


Ijapokuwa mwenye dhambi amefanya maovu mara mia na akazidisha siku zake; lakini hata hivyo najua hakika ya kwamba itakuwa heri kwao wamchao Mungu, wenye kicho mbele zake;


Ni nani miongoni mwenu amchaye BWANA, aitiiye sauti ya mtumishi wake? Yeye aendaye katika giza, wala hana nuru, naye alitumainia jina la BWANA, na kumtegemea Mungu wake.


Na rehema zake hudumu vizazi hata vizazi Kwa hao wanaomcha.


Kwa maana naifurahia sheria ya Mungu kwa utu wa ndani,


Kwa kuwa nia ya mwili ni mauti; bali nia ya roho ni uzima na amani.


Utabarikiwa mjini, utabarikiwa na mashambani.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo