Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Zaburi 11:6 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

6 Awanyeshee wasio haki mitego, Moto na kiberiti na upepo wa joto Na viwe fungu la kikombe chao.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

6 Atawanyeshea waovu makaa ya moto na madini ya kiberiti; upepo wa hari utakuwa ndio adhabu yao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

6 Atawanyeshea waovu makaa ya moto na madini ya kiberiti; upepo wa hari utakuwa ndio adhabu yao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

6 Atawanyeshea waovu makaa ya moto na madini ya kiberiti; upepo wa hari utakuwa ndio adhabu yao.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

6 Atawanyeshea waovu makaa ya moto mkali na kiberiti kinachowaka; upepo wenye joto kali ndio fungu lao.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

6 Atawanyeshea waovu makaa ya moto mkali na kiberiti kinachowaka, upepo wenye joto kali ndio fungu lao.

Tazama sura Nakili




Zaburi 11:6
25 Marejeleo ya Msalaba  

Ndipo BWANA akanyesha juu ya Sodoma na juu ya Gomora kiberiti na moto kutoka mbinguni kwa BWANA.


Wakapelekewa sehemu za chakula kutoka mezani pake, lakini akazidisha sehemu ya Benyamini iwe kubwa mara tano kuliko zao. Wakanywa, wakafurahi pamoja naye.


Amefichiwa tanzi chini, Na mtego amewekewa njiani.


Katika hema yake hakuna kitakachobaki; Kiberiti kitamwagwa juu ya makazi yake.


Hapo atakapo kulijaza tumbo lake, Mungu atamtupia ukali wa ghadhabu zake, Na kuunyesha juu yake akiwa anakula.


Badala ya mvua aliwapa mvua ya mawe, Na umeme uliomulika ghafla katika nchi yao.


BWANA ndiye fungu la posho langu, Na la kikombe changu; Wewe unayaamua maisha yangu.


BWANA alinguruma kutoka mbinguni, Yeye Aliye Juu akaitoa sauti yake, Mvua ya mawe na makaa ya moto.


Naye mtu mwovu ana mapigo mengi, Bali amtumainiaye BWANA fadhili zitamzunguka.


Maana mkononi mwa BWANA mna kikombe, Na mvinyo yake inatoka povu; Kumejaa machanganyiko; Naye huyamimina. Na sira zake wasio haki wa dunia Watazifyonza na kuzinywa.


Amka, amka, simama, Ee Yerusalemu, Wewe uliyenywea mkononi mwa BWANA, Kikombe cha hasira yake; Ukalinywea na kumaliza bakuli la kulevyalevya Umelinywea na kulimaliza.


BWANA, Bwana wako na Mungu wako, awateteaye watu wake, asema hivi, Tazama, nimeondoa mkononi mwako kikombe cha kulevyalevya, hilo bakuli la hasira yangu; hutalinywea tena;


Hiyo ndiyo kura yako, fungu lako ulilopimiwa na mimi, asema BWANA; kwa kuwa umenisahau, na kuutumainia uongo.


Basi Bwana MUNGU asema hivi; Nitaupasua kwa upepo wa dhoruba, katika ghadhabu yangu; tena kutakuwa mvua ya barafu ya kufurika katika hasira yangu; na mawe makubwa ya barafu katika hasira ya kuukomesha.


Nami nitamhukumu kwa tauni, na kwa damu; nami nitanyesha mvua ifurikayo, na mvua ya mawe makubwa sana, na moto na kiberiti juu yake, na vikosi vyake, na watu wa kabila nyingi walio pamoja naye.


Umejaa aibu badala ya utukufu; unywe nawe, uwe kama mtu asiyetahiriwa; kikombe cha mkono wa kulia wa BWANA kitageuzwa ukipokee, na aibu kuu itakuwa juu ya utukufu wako.


lakini siku ile Lutu aliyotoka Sodoma kulinyesha moto na kibiriti kutoka mbinguni vikawaangamiza wote.


Basi Yesu akamwambia Petro, Rudisha upanga alani mwake; je! Kikombe alichonipa Baba, mimi nisikinywee?


Hata siku ile ilipofika Elkana alipotoa dhabihu, kumpa mkewe Penina sehemu, akawapa na watoto wake wote, wanaume kwa wanawake, sehemu zao;


Samweli akamwambia mpishi, Lete ile sehemu niliyokupa, hiyo niliyokuambia, Iweke kando.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo