Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Zaburi 107:4 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

4 Walitangatanga jangwani katika njia ya nyika; Hawakuona mji wa kukaa.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

4 Baadhi walitangatanga katika jangwa tupu, wasiweze kufikia mji wa kukaa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

4 Baadhi walitangatanga katika jangwa tupu, wasiweze kufikia mji wa kukaa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

4 Baadhi walitangatanga katika jangwa tupu, wasiweze kufikia mji wa kukaa.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

4 Baadhi yao walitangatanga jangwani, hawakuona njia ya kuwafikisha mji ambao wangeweza kuishi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

4 Baadhi yao walitangatanga jangwani, hawakuona njia ya kuwafikisha mji ambao wangeweza kuishi.

Tazama sura Nakili




Zaburi 107:4
11 Marejeleo ya Msalaba  

Huwaondolea moyo wakuu wa watu wa nchi, Na kuwapoteza nyikani pasipokuwa na njia.


Aliwamwagia wakuu dharau, Na kuwazungusha katika nyika isiyo na njia.


Kama vile mchungaji atafutavyo kondoo wake, siku ile anapokuwa kati ya kondoo wake waliotawanyika; ndivyo nitakavyowatafuta kondoo wangu; nami nitawaokoa katika mahali pote walipotawanyika, katika siku ya mawingu na giza.


Kondoo wangu walitangatanga katika milima yote, na juu ya kila kilima kirefu; naam, kondoo wangu walitawanyika juu ya uso wote wa dunia; wala hapakuwa na mtu aliyewaulizia, wala kuwatafuta.


Kisha watoto wenu watakuwa wachungaji jangwani muda wa miaka arubaini nao watauchukua mzigo wa uasherati wenu, hadi maiti zenu zitakapoangamia jangwani.


Na hasira za BWANA ziliwaka juu ya Israeli, naye akawatembeza huku na huko jangwani muda wa miaka arubaini, hata kizazi hicho kizima kilichokuwa kimefanya uovu machoni pa BWANA kilipoisha angamia.


Alimkuta katika nchi ya ukame, Na katika jangwa tupu litishalo; Alimzunguka, akamtunza; Akamhifadhi kama mboni ya jicho;


aliyekuongoza katika jangwa lile kubwa lenye kitisho, lenye nyoka za moto na nge, nchi ya kiu isiyokuwa na maji; aliyekutolea maji katika mwamba mgumu,


(watu ambao ulimwengu haukustahili kuwa nao), walikuwa wakizungukazunguka katika nyika na katika milima na katika mapango na katika mashimo ya nchi.


Yule mwanamke akakimbilia nyikani, ambapo ana mahali palipotengenezwa na Mungu, ili wamlishe huko muda wa siku elfu moja mia mbili na sitini.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo