Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Zaburi 106:40 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

40 Hasira ya BWANA ikawaka juu ya watu wake, Akauchukia urithi wake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

40 Hasira ya Mwenyezi-Mungu ikawawakia watu wake, akachukizwa sana na hao waliokuwa mali yake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

40 Hasira ya Mwenyezi-Mungu ikawawakia watu wake, akachukizwa sana na hao waliokuwa mali yake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

40 Hasira ya Mwenyezi-Mungu ikawawakia watu wake, akachukizwa sana na hao waliokuwa mali yake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

40 Kwa hiyo Mwenyezi Mungu akawakasirikia watu wake na akauchukia sana urithi wake.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

40 Kwa hiyo bwana akawakasirikia watu wake na akauchukia sana urithi wake.

Tazama sura Nakili




Zaburi 106:40
14 Marejeleo ya Msalaba  

Naye akawa adui wa Israeli siku zote za Sulemani, zaidi ya madhara yake Hadadi; naye akawachukia Israeli, akamiliki juu ya Shamu.


Ee Mungu, mbona umetutupa milele? Kwa nini hasira yako inatoka moshi Juu ya kondoo wa malisho yako?


Nimeiacha nyumba yangu, nimeutupa urithi wangu; nimemtia mpenzi wangu katika mikono ya adui zake.


Bwana ameitupilia mbali madhabahu yake, Amepachukia patakatifu pake; Amezitia katika mikono ya hao adui Kuta za majumba yake; Wamepiga kelele ndani ya nyumba ya BWANA Kama katika sikukuu.


Nanyi msiende kwa kuzifuata desturi za taifa, niitoayo mbele yenu; kwa kuwa wao waliyafanya mambo hayo yote, na kwa ajili ya hayo niliwachukia.


Nami nitapaharibu mahali penu palipoinuka, na kuziangusha sanamu zenu za jua, nami nitaitupa mizoga yenu juu ya mizoga ya sanamu zenu; na roho yangu itawachukia.


Nami nikawakatilia mbali wachungaji watatu katika mwezi mmoja; maana nafsi yangu ilikuwa imechoka kwa ajili yao, na nafsi zao pia walinichukia.


BWANA akaona, akawachukia, Kwa sababu ya kukasirishwa na wanawe na binti zake.


Nao ni watu wako, urithi wako, uliowatoa kwa nguvu zako kuu na mkono wako ulionyoka.


Hasira ya BWANA ikawaka juu ya Israeli, naye akawatia katika mikono ya watu waliowateka nyara, akawauza na kuwatia katika mikono ya adui zao pande zote; hata wasiweze tena kusimama mbele ya adui zao.


Basi hasira ya BWANA ikawaka juu ya Israeli, naye akasema, Kwa kuwa taifa hili limelivunja agano langu nililowaamuru baba zao, wala hawakuisikiliza sauti yangu;


Kwa hiyo hasira za BWANA ziliwaka juu ya Israeli, naye akawauza na kuwatia mikononi mwa Kushan-rishathaimu mfalme wa Mesopotamia; na wana wa Israeli wakamtumikia huyo Kushan-rishathaimu muda wa miaka minane.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo