Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Zaburi 106:34 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

34 Hawakuwaangamiza watu wa nchi Kama BWANA alivyowaambia;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

34 Hawakuwaua watu wa mataifa mengine kama Mwenyezi-Mungu alivyowaamuru.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

34 Hawakuwaua watu wa mataifa mengine kama Mwenyezi-Mungu alivyowaamuru.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

34 Hawakuwaua watu wa mataifa mengine kama Mwenyezi-Mungu alivyowaamuru.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

34 Hawakuyaangamiza yale mataifa kama Mwenyezi Mungu alivyowaagiza,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

34 Hawakuyaangamiza yale mataifa kama bwana alivyowaagiza,

Tazama sura Nakili




Zaburi 106:34
18 Marejeleo ya Msalaba  

wa watoto wao waliosalia baada yao katika nchi, ambao wana wa Israeli hawakuwakomesha, katika hao Sulemani akawatumikisha shokoa hata leo.


ndipo mtakapowafukuza wenyeji wote wa hiyo nchi mbele yenu, nanyi mtayaharibu mawe yao yote yenye kuchorwa sanamu, na kuziharibu sanamu zao zote za kusubu, kuvunjavunja mahali pao pote palipoinuka;


Nawe angamiza mataifa yote atakayokupa BWANA, Mungu wako; jicho lako lisiwahurumie, wala usiitumikie miungu yao; kwani jambo hilo litakuwa ni mtego kwako.


wakati BWANA, Mungu wako, atakapowatoa mbele yako, nawe utawapiga; wakati huo ndipo uwaondoe kabisa; usifanye agano nao, wala kuwahurumia; wala usioane nao;


Tena katika habari ya Wayebusi, hao wenye kukaa Yerusalemu, wana wa Yuda hawakuweza kuwatoa; lakini hao Wayebusi walikaa pamoja na wana wa Yuda huko Yerusalemu hata hivi leo.


Nao hawakuwatoa Wakanaani waliokuwa wakikaa Gezeri; lakini hao Wakanaani waliketi kati ya Efraimu, hata hivi leo, wakawa watumishi wa kufanya kazi za shokoa.


BWANA alikuwa pamoja na Yuda; naye akawafukuza watu waliokaa katika nchi yenye milima; asiweze kuwafukuza hao waliokaa katika hilo bonde, kwa kuwa wao walikuwa na magari ya chuma.


Lakini wana wa Benyamini hawakuwafukuza Wayebusi waliokaa mji wa Yerusalemu; bali Wayebusi walikaa pamoja na wana wa Benyamini ndani ya Yerusalemu hata hivi leo.


nanyi msifanye agano lolote na hawa wenyeji wa nchi hii; yabomoeni madhabahu yao; lakini hamkuisikia sauti yangu; je! Mmefanya haya kwa sababu gani?


Basi sasa nenda ukawapige Waamaleki, na kuviharibu kabisa vitu vyote walivyonavyo, wala msiwaachilie; bali waueni, mwanamume na mwanamke, na mtoto anyonyaye, ng'ombe na kondoo, ngamia na punda.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo