Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Zaburi 103:8 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

8 BWANA amejaa huruma na neema, Haoni hasira upesi, ni mwingi wa fadhili.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

8 Mwenyezi-Mungu ni mwenye rehema na huruma; ni mvumilivu na mwingi wa fadhili.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

8 Mwenyezi-Mungu ni mwenye rehema na huruma; ni mvumilivu na mwingi wa fadhili.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

8 Mwenyezi-Mungu ni mwenye rehema na huruma; ni mvumilivu na mwingi wa fadhili.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

8 Mwenyezi Mungu ni mwingi wa huruma na mwenye neema; si mwepesi wa hasira, bali amejaa upendo.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

8 bwana ni mwingi wa huruma na mwenye neema; si mwepesi wa hasira, bali amejaa upendo.

Tazama sura Nakili




Zaburi 103:8
17 Marejeleo ya Msalaba  

ila wakakataa kutii, wala hawakuyakumbuka maajabu yako, uliyoyafanya kati yao; lakini wakafanya shingo zao kuwa ngumu, na katika kuasi kwao wakaweka jemadari, ili wairudie hali ya utumwa; lakini wewe u Mungu, uliye tayari kusamehe, mwenye neema, mwenye huruma nyingi, si mwepesi wa hasira, u mwingi wa rehema, basi hukuwaacha.


Ee Israeli, umtarajie BWANA; Maana kwa BWANA kuna fadhili, Na kwake kuna ukombozi mwingi.


BWANA ni mwenye fadhili na huruma, Si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa rehema,


Utawasitiri kutoka kwa fitina za watu Katika maficho ya kuwapo kwako; Utawaficha katika hema Na ushindani wa ndimi.


Lakini Wewe, Bwana, U Mungu wa rehema na neema, Mvumilivu, mwingi wa fadhili na kweli.


Kwa maana Wewe, Bwana, U mwema, Umekuwa tayari kusamehe, Na mwingi wa fadhili, Kwa watu wote wakuitao.


Mtu mbaya na aache njia yake, Na mtu asiye haki aache mawazo yake; Na amrudie BWANA, Naye atamrehemu; Na arejee kwa Mungu wetu, Naye atamsamehe kabisa.


wewe uwarehemuye watu elfu nyingi, uwalipaye baba za watu uovu wao vifuani mwa watoto wao baada yao; Mungu aliye mkuu, aliye hodari, BWANA wa majeshi ndilo jina lake;


rarueni mioyo yenu, wala si mavazi yenu, mkamrudie BWANA, Mungu wenu; kwa maana yeye ndiye mwenye neema, amejaa huruma; si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa rehema, naye hughairi kuadhibu.


Akamwomba BWANA, akasema, Nakuomba, Ee BWANA; sivyo hivyo nilivyosema, hapo nilipokuwa katika nchi yangu? Hii ndiyo sababu nilifanya haraka kukimbilia Tarshishi; kwa maana nilijua ya kuwa wewe u Mungu mwenye neema, umejaa huruma, si mwepesi wa hasira, u mwingi wa rehema, nawe waghairi mabaya.


BWANA si mwepesi wa hasira, ana uweza mwingi, wala hatamhesabia mtu mwovu kuwa hana hatia kamwe; BWANA ana njia yake katika kisulisuli na tufani, na mawingu ni mavumbi ya miguu yake.


BWANA ni mpole wa hasira, mwingi wa rehema, mwenye kusamehe uovu na makosa, naye hatamfanya mwenye hatia kuwa hana makosa kwa njia yoyote; mwenye kuwapatiliza wana kwa uovu wa baba zao, katika kizazi cha tatu na cha nne.


nami nawarehemu maelfu wanipendao, na kuzishika amri zangu.


Angalieni, twawaita heri wao waliostahimili. Mmesikia habari za kustahimili kwake Ayubu, kuona mwisho Bwana aliyomtendea, jinsi Bwana alivyo mwingi wa rehema na mwenye huruma.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo